Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha majina ya makocha 40 wa Tanzania kushiriki katika kozi ya ukocha ya leseni B ya shirikisho hilo. Makocha wote waliopitishwa wana cheti cha ukocha cha ngazi pevu (advance). Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ni miongoni mwa makocha hao watakaoshiriki kozi hiyo itakayofanyika jijini …
Dk. Shein kufunga Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kufunga michuano ya 35 ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoendelea jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF leo Dar es Salaam, sherehe za ufungaji wa mashindano hayo yaliyoshirikisha mataifa 10 wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika …
Zanzibar, Burundi wafungasha virago Tusker Chalenji
*Sudan, Rwanda wakata tiketi Nusu Fainali Na Mwandishi Wetu WAKATI timu za taifa za Sudan na Rwanda zikikata tiketi za kuingia Nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji jana Timu ya taifa ya Zanzibar imeungana na Burundi na kuyaanga mashindano hayo baada ya kukubali kichapo katika michezo miwili ya jana. Mchezo wa kwanza timu ya Sudan ilifanikiwa kuingia …
Robo fainali Kombe la CECAFA Tusker Challenge leo
MICHUANO ya Robo fainali Kombe la CECAFA Tusker Chalenji inaanza leo Desemba 5,2011 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura jana kwa vyombo vya habari leo zitapigwa mechi mbili mfululizo. Wambura amesema mechi hizo mbili ambazo zitafanyika Uwanja wa Taifa, Dar …
Tanzania chup chup kutolewa Tusker Chalenji
Na Joachim Mushi TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) hatimaye imefanikiwa kuendelea ki-bahati nasibu na hatua ya pili katika Mashindano ya Kombe la Tusker Chalenji baada ya fufungwa mabao 2-1 na timu ya Taifa ya Zimbabwe jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars imeponea chup chup baada ya kufanikiwa kufunga bao moja katika mchezo …
Ngorongoro Heroes yaanza kwa sare
Na Mwandishi Wetu TANZANIA (Ngorongoro Heroes) imeanza kwa sare michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa vijana chini ya miaka 20 inayofanyika Gaborone, Botswana. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, kupitia kwa Ofisa Habari wake, Boniface Wambura ni kwamba, mchezo wa Desemba 2 mwaka huu dhidi ya mabingwa watetezi Zambia uliofanyika Uwanja …