*Wabunge wanawake nao wawachakaza Wawakilishi netibali Na Joachim Mushi TIMU ya mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania leo imeiadhibu bila huruma Timu ya mpira wa miguu ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar (BLW) baada ya kuichapa mabao 4 kwa 1. Timu ya Bunge ambayo iliongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja (Mb) akicheza …
Tanzania yautema ubingwa CECAFA Tusker Chalenji
*Yachapwa 3-1 na Waganda, mashabiki Yanga washerekea Na Joachim Mushi TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars jana imetolewa kuingia fainali katika Mashindano ya Kombe la Tusker baada ya kukubali kichapo cha mabao 3 kwa moja (3-1) kutoka kwa majirani zao wa Uganda. Kwa matokeo hayo Tanzania imeshindwa kutetea Ubingwa ambao ilikuwa ikiushikiliwa wa kikombe hocho cha CECAFA Tusker …
Ngorongoro Heroes kurejea nchini Nov 9
Na Mwandishi Wetu, Gaborone TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inatarajia kurejea nyumbani kesho Ijumaa alfajiri ikitokea jijini hapa ambapo ilikuwa inashiriki kwenye mashindano ya vijana ya COSAFA ambayo leo yanaingia katika hatua ya nusu fainali. Ngorongoro Heroes iliyokuwa kwenye kundi ‘C’ ilimaliza hatua ya makundi ikiwa katika nafasi ya pili …
Nusu Fainali CECAFA Tusker Chalenji kesho
Na Mwandishi Wetu MECHI mbili za nusu fainali kuwania ubingwa wa 35 wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zinachezwa kesho (Desemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF, jijini Dar es Salaam na Ofisa Habari …
Serengeti Breweries yadhamini pambano la wabunge Vs Wawakilishi
*Pambano kufanyika 9 Desemba kati ya Wabunge na Wawakilishi Na Joachim Mushi KAMPUNI ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imetangaza udhamini wa pambano la kihistoria la mpira wa miguu na wa mikono ‘netball’ kati ya timu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania na ile ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW) Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam …
Tanzania yatinga Nusu Fainali Tusker Chalenji
Na Joachim Mushi TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars imetinga hatua ya Nusu Fainali baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Malawi bao 1-0, katika mchezo mkali na wa kuvutia uliyofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Kilimanjaro Stars ambayo ilicheza kwa kujihami mchezo huo, mpaka inakwenda mapumziko, ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na mchezaji …