Kozi ya makamishna kuanza kesho

KOZI kwa ajili ya makamishna wa mechi za Ligi Kuu na mashindano mengine yanayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inafanyika kesho (Desemba 28 mwaka huu) na keshokutwa (Desemba 29 mwaka huu). Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa leo na TFF, washiriki wa kozi hiyo itakayofanyika ofisi za TFF ni wale wanaoomba kwa mara ya kwanza (beginners), na …

Usajili mashindano ya Klabu CAF

*FIFA yamteua Minja kusimamia mechi SHUGHULI ya usajili kwa ajili ya timu za Tanzania zitakazoshiriki michuano ya ngazi ya klabu Afrika inayosimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) inaendelea. Yanga itacheza Ligi ya Mabingwa (CL) wakati Simba itashindana katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CC). Kwa upande wa Yanga hadi sasa imeshawasilisha Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania …

Yanga Tabata kukutana Boxing Day

Na Mwandishi Wetu WANACHAMA wa klabu ya Yanga tawi la Tabata wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa mwaka utakaofanyika kesho, Jumatatu (26 Desemba, 2011) kwenye Ukumbi wa Ofisa Mtendaji Kata huku ajenda kubwa ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa tawi hilo, Michael Warioba alisema, wanachama …

YAYA TOURE mchezaji bora CAF

Mcheza kiungo wa klabu ya Manchester City na Timu ya Taifa ya Ivory Coast,Yaya Toure amechaguliwa kua mchezaji bora wa soka na Shirikisho la soka ya Afrika(CAF) Mchezaji huyo mashuhuri alipitia mchujo wa ushindani na Seydou Keita kutoka Mali anayechezea klabu ya Barcelona na Andre Ayew wa Ghana pia klabu ya Olympique Marseille. Toure, mwenye umri wa miaka 28, alichaguliwa …

Simba, Yanga kuchangia wahanga wa mafuriko

KLABU za Yanga na Simba zitacheza mechi za kimataifa za kirafiki na mabingwa wa Malawi, Escom United siku ya Jumatatu na Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya kuchangia watu waliokumbwa na janga la mafuriko jijini Dar es Salaam. Kwa siku tatu mfululizo sasa mvua kubwa zimekuwa zikinyesha jijini Dar es Salaam na kusababisha baadhi ya watu kufariki, wengine …

Mtanzania aombewa ITC Uingereza

*Mzambia kuichezesha Twiga Stars CHAMA cha Mpira wa Miguu Uingereza (FA) kimetuma maombi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kumuombea Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) mchezaji Douglas Didas Masaburi ili ajiunge na klabu ya nchini humo. Masaburi mwenye umri wa miaka 21 anaombewa ITC ili ajiunge na klabu ya Coventry Spartans akiwa mchezaji wa ridhaa. Coventry Spartans iko …