MECHI ya marudiano kusaka tiketi ya kucheza fainali za Nane za Kombe Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia itachezeshwa na waamuzi kutoka Zimbabwe. Waamuzi katika mechi hiyo itakayofanyika Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam watakuwa Rusina Majo Kuda (mwamuzi wa kati) wakati waamuzi wasaidizi …
ZH Poppe yatoa tiketi kwa waamuzi
KAMPUNI ya ZH Hope Limited imegharamia tiketi za waamuzi na kamishna atakayesimamia mechi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Namibia itakayofanyika Januari 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Mbali ya tiketi hizo za ndege, pia kampuni hiyo itagharamia hoteli (malazi na chakula) kwa kamishna na waamuzi hao …
Ligi Kuu ya Vodacom kuanza Jumamosi
Na Mwandishi Wetu MZUNGUKO wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza keshokutwa (Januari 21 mwaka huu) kwa mechi nne. Moro United itaikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Mtibwa Sugar itaoneshana kazi na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani. Nayo Toto Africans itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa …
SBC Tanzania waisaidia Twiga Stars vinywaji
Na Mwandishi Wetu TIMU ya Taifa ya wanawake Twiga Stars Januari 17 mwaka huu imekabidhiwa msaada wa maji ya kunywa na soda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yake ya marudiano dhidi ya Namibia itakayochezwa Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kampuni ya SBC Tanzania inayozalisha Pepsi, Mirinda na 7up ilikabidhi msaada wa vinywaji hivyo …
Arsenal yalala, Newcastle yaibuka
MATUMAINI ya Timu ya Arsenal kusogelea nafasi nne bora za juu za Ligi ya Soka ya Uingereza yamevurugwa na Timu ya Swansea baada ya kuonesha kandanda murua na kuweza kupata pointi tatu muhimu kwa kuilaza Arsenal mabao 3-2 katika mchezo wa kusisimua. Katika mchezo huo Arsenal ndio walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya nne kwa bao la Robin …
Dk Shein aipongeza kamati ya Mapinduzi Cup 2012
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, ameipongeza Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mapinduzi ‘Mapinduzi Cup 2012’ kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa kitaifa. Dk. Shein ametoa pongezi hizo leo alipokuwatana na Wajumbe wa kamati hiyo, pamoja na wafadhili wakubwa wa mashindano ya mwaka huu ambayo yalifikia kilele Januari …