Wakala asema Balotelli anaonewa England

WAKALA wa Mario Balotelli ameonya mshambuliaji huyo anaweza kuachana na kandanda ya England iwapo ataendelea kutotendewa haki katika matukio mbalimbali. Balotelli, anakabiliwa na adhabu ya kutocheza michezo minne baada ya kushtakiwa na Chama cha Kandanda cha England kwa kitendo cha vurugu. Mshambuliaji huyo wa Manchester City alionekana kumkanyaga kichwani Scott Parker kabla ya kufunga bao la ushindi kwa mkwaju wa …

TFF yataja viingilio mechi ya Twiga Stars na Namibia

KIINGILIO cha chini kwa mechi ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Twiga Stars na Namibia itakayochezwa Jumapili, Januari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 2,000. Kiwango hicho ni kwa washabiki kwa viti vya bluu na kijani. Viti hivyo kwa pamoja vinachukua jumla ya watazamaji 36,693 kwenye uwanja huo wenye uwezo …

Yanga yatakiwa kumlipa Njoroge sh. mil 17

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kupitia kitengo chake cha utatuzi wa migogoro (Dispute Resolution Chamber- DRC) limeagiza klabu ya Yanga kumlipa mchezaji John Njoroge sh. 17,159,800 ikiwa ni fidia kwa kuvunja mkataba wake kinyume cha taratibu. Uamuzi huo wa DRC chini ya Jaji Theo van Seggelen ambaye ni raia wa Uholanzi ulifanywa Desemba 7 …

Ivory Coast yaiadhibu Angola AFCON

TIMU ya mpira wa Miguu ya Ivory Coast imeanza kampeni ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi dhidi ya Sudan walionekana kusumbua. Nahodha Didier Drogba alifunga bao kwa kichwa kutokana na krosi iliyochongwa na Salomon Kalou, lakini haukuwa ushindi wa kujivunia sana kwa timu inayopewa nafasi kubwa ya kunyakua kombe hilo. Sudan itakuwa imefurahi kutokana na kandanda iliyoonesha …

Wabunge kucheza pambano kuchangia Twiga Stars

*TFF yaomba kutumia uwanja wa taifa bure WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia timu ya Bunge wameomba kucheza mechi maalumu dhidi ya Twiga Stars kabla ya kuwasilisha mchango wao kwa timu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kupitia kwa Ofisa Habari wake Boniface Wambura amesema benchi la …

Man City yaendelea kupaa, Man U yaifanyia vibaya Arsenal

MSHAMBULIAJI, Mario Balotelli amejitokeza kuwa kiini cha mgogoro na sababu ya kuipatia ushindi Manchester City ikipiga hatua dhidi ya mshindani wake wa karibu Manchester United. Balotelli aliingia wakati Manchester City ikisukumwa na Tottenham 2-2 baada ya kurudisha mabao mawili katika kipindi kifupi ikionekana kuondoka na angalau pointi moja. Wakati ikionekana kua Manchester City imepungukiwa na maarifa Bario Balotelli aliangushwa ndani …