NCHI zote mbili wenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), yaani Gabon na Equatorial Guinea tayari zimefuzu kuingia hatua ya Robo Fainali za mashindano hayo. Gabon ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-2 katika dakika ya mwisho, ilipocheza dhidi ya Morocco siku ya Ijumaa, na kufuzu kuingia robo fainali katika mashindano ya AFCON. Mechi hiyo ilichezewa mjini Libreville. …
Pambano la Yanga na Zamalek kuchezeshwa na Waethiopia
Na Mwandishi Wetu WAAMUZI kutoka Ethiopia ndiyo watakaochezesha mechi namba 7 ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misri itakayochezwa Februari 18 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na TFF, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Bamlack Tessema kuwa mwamuzi wa kati …
JKT Ruvu, Yanga kucheza saa 12 jioni
Na Mwandishi Wetu MECHI namba 100 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Yanga itachezwa kesho (Januari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo. Lakini mechi hiyo sasa itaanza saa 12 kamili jioni badala ya saa 10 kamili jioni. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface …
Tamasha la kuvumbua vipaji Dar (Grassroot)
Na Mwandishi Wetu TAMASHA la mafunzo ya kuhamasisha watoto kucheza mpira wa miguu na kuvumbua vipaji (Grassroot) kwa shule maalum zilizochaguliwa katika Mkoa wa Dar es Salaam linaendelea Februari 3 mwaka huu. Siku hiyo tamasha hilo litafanyika katika Shule ya Msingi Mtoni Kijichi wilayani Temeke kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. Februari 10 mwaka huu tamasha lingine litafanyika …
Simba kuchezeshwa na Warundi Kigali
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Burundi kuchezesha mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Kiyovu Sport ya Rwanda itakayochezwa jijini Kigali. Waamuzi hao ni Thierry Nkurinziza atakayekuwa katikati wakati wasaidizi wake ni Jean-Claude Birumushahu na Jean-Marie Hakizimana. Mwamuzi wa akiba atakuwa Hudu Munyemana kutoka Rwanda. Kamishna wa mechi …