Na Mwandishi Wetu MZUNGUKO wa 16 wa Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza Februari 4 mwaka huu kwa mechi tatu. Coastal Union itakuwa mgeni wa Moro United kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam. Nayo Villa Squad itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Ruvu Shooting na Polisi Dodoma …
Simba, JKT Oljoro zavuna mil 40
PAMBANO la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Oljoro JKT lililochezwa Februari Mosi mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 40,191,000. Jumla ya watazamaji waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 105 kwa kiingilio cha sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000 kwa VIP A walikuwa 11,860. Taarifa ya TFF leo kwa vyombo vya …
Wambura aendelea kuitesa TFF
Na Joachim Mushi SUALA la mgogoro wa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Mara (FAM), Michael Wambura ambaye baadaye alienguliwa na Kamati ya Uchaguzi TFF limeendelea kulikanganya shirikisho hilo, na sasa imeamua kuomba msaada wa kisheria. Jana Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Oseah ameamua kuiandikia barua Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za …
Wamisri kuichezesha Stars Februari 29
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri kuchezesha mechi ya kwanza ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za 29 za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Msumbiji. Waamuzi watakaochezesha mechi hiyo namba 25 itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni Farouk Mohamed atakayekuwa mwamuzi …
Nahodha Twiga Stars kucheza Uturuki
*Twiga Stars yaingiza mil 38 NAHODHA wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars), Sophia Mwasikili ameondoka Januari 30 mwaka huu kwa ndege ya Turkish Airlines kwenda Uturuki kucheza mpira wa kulipwa. Mwasikili amekwenda kujiunga na Luleburgazgucu Spor Kulubu inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ya Wanawake nchini humo. Beki huyo wa kati wa Twiga Stars aliyekuwa …