Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Israel Mujuni wa Tanzania ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya marudiano ya raundi ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya APR ya Rwanda na Tusker ya Kenya itakayochezwa jijini Kigali kati ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu. Mujuni atasaidiwa na Samuel Mpenzu na Khamis Maswa kutoka …
TFF yasusha viingilio Uwanja wa Chamazi-AZAM
*Simba Vs Villa waingiza mil 30/- SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanyia marekebisho viingilio vya mechi za Ligi Kuu ya Vodacom zitakazochezwa katika Uwanja wa Azam ulioko eneo la Chamazi, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi za uwanja huo sasa vitakuwa sh. 1,000 kwa mzunguko na sh. 5,000 kwa jukwaa kuu badala ya vile vya awali vya sh. …
Zambia na Ivory Coast zatinga nusu fainali
ZAMBIA sasa itacheza na Ghana au Tunisia katika nusu fainali. Zambia ilikuwa timu ya kwanza kujitengea nafasi katika nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika katika mechi ya Jumamosi, baada ya pambano la kwanza la robo fainali kati yake na Sudan, na ilipoondoka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi iliyochezewa uwanja wa Bata. Stoppila Sunzu aliandikisha bao la …
TFF yaomboleza kifo cha GRATIAN MATOVU
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mwamuzi wa zamani wa kimataifa Gratian Matovu kilichotokea saa 6 mchana Februari 3 mwaka huu nyumbani kwake Mbezi Beach Makonde, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari leo, inasema licha ya kuwa mwamuzi, Matovu aliyezaliwa Novemba Mosi …
John Terry avuliwa unahodha wa England
CHAMA cha Soka nchini Uingereza kimemvua unahodha mchezaji John Terry wa timu ya Taifa ya England. Chama hicho cha soka kinasema Terry hapaswi kushika unahodha wa timu ya taifa hadi pale kesi inayomkabili ya madai ya kumtamkia matusi ya kibaguzi mchezaji mweusi mwaka jana. Hata hivyo chama cha soka Uingereza kimesema anaweza kubakia katika timu ya taifa. Analaumiwa kwa kumtamkia …
Mtihani wa mawakala wa wachezaji FIFA Machi 29
Na Mwandishi Wetu MTIHANI wa uwakala wa wachezaji (players agent) wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Alhamisi ya Machi 29 mwaka huu saa 10 kamili asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura jijini Dar es Salaam, kutakuwa na jumla ya …