Zambia na Ivory Coast kuvaana fainali AFCON

IVORY Coast itakutana na Zambia kwenye Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya timu hizo mbili kushinda mechi zao za nusu fainali. Ivory Coast imefuzu baada ya kuishinda Mali 1-0 katika nusu fainali yao mjini Libreville, nchini Gabon. Bao la ushindi la Ivory Coast lilifungwa na mchezaji wa Arsenal Gervinho katika kipindi cha pili. Awali katika mji …

Sababu ya kujiuzulu kwa kocha Capello!

ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Uingereza (England), muitalia, Fabio Capello amejiuzulu rasmi kuifundisha timu hiyo. Capello amefikia hatua hiyo jana baada ya kufanya mkutano wa takribani saa nzima na viongozi wakuu wa Chama Cha Soka cha Uingereza (FA). Mkutano huo uliowahusisha Mwenyekiti wa FA, David Bernstein, Katibu Mkuu wake, Alex Horne pamoja na …

Breaking Newz; Kocha wa Uingereza ajiuzulu

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uingereza (England), fabio Capello amejiuzulu kuifundisha timu hiyo. Taarifa ambayo mtandao huu umezipata muda si mrefu ni kwamba, kocha huyo kafikia hatua ya kujiuzulu kwa kile Nahodha wa timu hiyo, John Terry kuvuliwa nafasi hiyo bila yeye kuhusishwa. Taarifa zaidi za sababu nyingine tutawaleteeni hapo baadaye.

Victor Mgimwa aombewa ICT nchini Thailand

MSHAMBULIAJI, Michael Victor Mgimwa ameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili acheze soka nchini Thailand. Chama cha Mpira wa Miguu cha Thailand (FAT) limetuma maombi hayo jana (Februari 6 mwaka huu) kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kupata hati hiyo. Mgimwa ambaye tayari yuko Thailand ameombewa hati hiyo ili aweze kuichezea timu ya Roiet FC ambayo …

Yanga kuonja sukari ya Mtibwa?

Na Mwandishi Wetu LIGI Kuu ya Vodacom ambayo iko katika raundi ya 16 inaendelea kesho kwa mechi moja kati ya Yanga na Mtibwa Sugar. Mechi hiyo namba 112 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni. Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga wakati wasaidizi wake ni Michael Mkongwa kutoka Iringa na Kudura Omary …