Libreville TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Zambia maarufu kama ‘Chipolopolo’ imetimiza ahadi iliyoitoa juzi wakati wakiwakumbuka wachezaji wenzao waliokufa kwa ajali ya ndege mwaka 2003, kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) leo. Chipolopolo imefanikiwa kutwaa kombe hilo baada ya kuwafunga timu ya Taifa ya Ivory Coast kwa mabao nane kwa saba …
Simba yapigwa faini, Mafisango aonywa
Na Mwandishi Wetu KAMATI ya Ligi imeagiza mchezaji Patrick Mafisango wa Simba aandikiwe barua ya onyo kutokana na kumsukuma mwamuzi Isihaka Shirikisho baada ya kumuonesha kadi nyekundu mchezaji mwenzake Haruna Moshi kwenye mechi kati ya Simba na JKT Oljoro. Nayo klabu ya Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 baada ya washabiki wake kurusha makopo ya soda na chupa za maji …
Waamuzi, Kamishna waondolewa Ligi Kuu Vodacom
Na Mwandishi Wetu WAAMUZI watatu na kamishna mmoja wameondolewa kuchezesha na kusimamia mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na kuonesha upungufu katika uchezeshaji na usimamizi. Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana Februari 11 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine ilipitia taarifa za waamuzi na makamishna wa VPL ambayo Februari 12 mwaka huu inaendelea katika raundi …
Klabu za Zamalek, Kiyovu Sport zaigomea Yanga na Simba
Na Mwandishi Wetu KLABU za Zamalek ya Misri na Kiyovu Sport zimekataa maombi ya mechi zao za marudiano za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga na Simba kusogezwa mbele kwa wiki moja kutoka wikiendi ya Machi 2, 3 na 4 mwaka huu. Taarifa ambazo mtandao huu umezipata leo kutoka kwa Ofisa Habari wa TFF, Bonifasi Wambura …
Kozi ya makocha angazi pevu yaahirishwa
Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeahirisha kozi ya ukocha ngazi pevu (Advanced Level) iliyokuwa ifanyike jijini Dar es Salaam kuanzia Februari 12- 25 mwaka huu. Kozi hiyo imeahirishwa kwa vile wengi wa makocha walioomba hawakufikia vigezo vilivyowekwa. Vigezo vya msingi vilikuwa mwombaji awe na cheti cha ukocha ngazi ya kati (Intermediate Level), wawe wanafanya kazi …
Ligi Kuu Vodacom 2011/12, timu 10 kibaruani kesho
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi ya 17 kesho, Februari 11 mwaka huu kwa mechi tano huku ile ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar iliyokuwa ichezwe Februari 12 mwaka huu ikilazimika kusogezwa mbele kwa siku moja. Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ametaja mechi za …