TFF yafanya marekebisho ratiba ya VPL

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho madogo kwenye ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupisha mechi mbili za Taifa Stars zinazotarajiwa kuchezwa Februari 23 na 29 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) ambayo itafanyika Februari 23 mwaka huu wakati ile ya mashindano …

AFC Arusha nayo yashushwa Daraja

Na Mwandishi Wetu TIMU ya AFC ya Arusha imeshindwa kutokea kwenye mechi ya Kundi C ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) dhidi ya 94 KJ iliyokuwa ichezwe Februari 15 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani. Kwa mujibu wa Kanuni ya 21 ya FDL timu yoyote inayoshindwa kufika kituoni na kusababisha mchezo husika kutochezwa itashushwa daraja hadi …

Kocha Poulsen ataja 23 watakaoivaa Msumbiji

KOCHA wa timu ya Taifa (Taifa Stars), Jan Poulsen Februari 16 mwaka huu ametangaza kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambalo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini. Amesema kabla ya kuivaa Msumbiji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi itakayochezwa Februari 29 mwaka huu, kikosi hicho …

Ligi Kuu Vodacom kuunguruma tena leo

LIGI Kuu ya Vodacom inaingia raundi ya 18 leo Februari 15 mwaka huu kwa mechi nne zitakazochezwa viwanja vya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha, Azam Chamazi jijini Dar es Salaam, Mkwakwani jijini Tanga na Kaitaba mjini Bukoba. Mwamuzi Israel Mujuni atazichezesha JKT Oljoro na Ruvu Shooting jijini Arusha, Azam na Villa Squad zitachezeshwa na Judith Gamba jijini Dar es …

TFF yaomboleza kifo cha Kassim Kashulwe

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha aliyewahi kuwa mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Kassim Kashulwe kilichotokea Februari 9 mwaka huu nyumbani kwake Kigurunyembe mkoani Morogoro. Licha ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF (wakati huo Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania- FAT), pia Kashulwe aliwahi kuwa …

Yanga, Ruvu shooting waingiza mil 47.5

Na Mwandishi wetu WATAZAMAJI 14,150 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Ruvu Shooting lililochezwa jana (Februari 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kuingiza sh. 47,554,000. Hata hivyo ni watazamaji saba tu waliokata tiketi za VIP A zilizokuwa zikiuzwa sh. 15,000. Viingilio vingine vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP B …