Na Mwandishi Wetu MAKOCHA Jan Poulsen wa Tanzania (Taifa Stars) na Gert Josef Angels wa Msumbiji (Mambas) leo, Februari 28 mwaka huu watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya timu zao. Taifa Stars na Mambas zinatarajia kukiputa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni katika mechi ya kwanza ya mchujo …
Prime Time Promotions yaingia mkataba na Simba
KLABU ya soka ya Simba ina furaha kubwa kuutangazia umma wa Watanzania kwamba imeingia mkataba na kampuni ya Prime Time Promotions/Clouds Media Group unaohusiana na Promosheni na Masoko (Promotion and Marketing) kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho (CAF) kati ya Simba na Kiyovu Sport ya Rwanda. Ushirikiano huo wa namna ya kipekee una lengo la kuhakikisha kuwa Watanzania …
‘Mambas’ wa Msumbiji kutua Dar leo
Na Mwandishi Wetu TIMU ya Taifa ya Msumbiji (Mambas) itawasili nchini kesho (Februari 26 mwaka huu) kwa ndege ya South African Airways. Ndege hiyo yenye mruko namba SA 186 inatarajia kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7.55 mchana. Msafara wa Mambas kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumatano ya Februari 29 mwaka …
Yanga yapewa masharti ya mchezo na Zamalek
*40 pekee watakiwa kwenda uwanjani Na Mwandishi Wetu MSAFARA wa Yanga utakaokuwa uwanjani kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek itakayochezwa wikiendi ijayo nchini Misri unatakiwa kuwa na watu wasiozidi 40. Kwa mujibu wa maelekezo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) yaliyotumwa jana Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ni …
Viingilio Stars na Msumbiji
KIINGILIO cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) itakayochezwa Februari 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000. Jumla viti 36,693 (rangi ya bluu na kijani) ndivyo vitakavyotumika kwa kiingilio hicho katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000 wakiwa wameketi. Viingilio …
Kozi ya madaktari wa tiba ya michezo
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa kozi ya awali ya madaktari au wataalamu wa viungo (physiotherapist) kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza itakayofanyika jijini Dar es Salaam. Kozi hiyo ya siku tano itakayoanza Machi 5-9 mwaka huu itakuwa na washiriki 32 tu. Kila klabu inatakiwa kutuma mshiriki mmoja ambapo anatakiwa kuwa daktari wa timu …