Na Vero Ignatus, Arusha JAJI wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Dkt. Modesta Opiyo amewapa siku kumi (10) mawakili wa mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema wawe wamewasilisha notisi ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama ya chini iliyomnyima dhamana Lema. Agizo hilo limekuja kutokana na mahamama kutoridhishwa na hoja za maombi ya mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa serikali dhidi ya taarifa ya dharura ya …
Kampuni ya TTCL Kuanza Kutoa Huduma za Kifedha
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujipanga na kuanza mkakati wa kutangaza huduma za fedha ambazo zitatolewa na kampuni hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao. Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma hiyo ambayo itaongeza ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani Dodoma. “Lazima …
Jeshi la Polisi Lamtia Mbaroni Tapeli Dar
Na Dotto MwaibaleJESHI la Polisi nchini limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa utapeli anayejulikana kwa jina la Wilfred Masawe (36) , Kabila mchaga na mkazi wa Buza, Temeke jijini Dar es Salaam. Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidi wa Polisi (ACP), Advera Bulimba amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu mbalimbali …
Rais Magufuli Ateuwa Wenyeviti 7 wa Bodi za Taasisi za Serikali
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya uteuzi wa Wenyeviti 7 wa Bodi za Taasisi za Serikali, na pia ameteua Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania na Mjumbe mmoja wa Baraza la Taifa la Biashara. Taarifa iliyotolewa leo tarehe 19 Desemba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imewataja walioteuliwa kama ifuatavyo; …
Barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu Kujengwa kwa Lami
SERIKALI imesema ipo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Loliondo- Mto wa Mbu yenye urefu wa KM 218 itakayojegwa kwa kiwango cha lami ili kurahishisha usafiri na usafirishaji wa mizigo kwa wananchi wa mikoa ya Mara, Manyara, Arusha na Mwanza. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji cha …