
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon baada ya Mkutano wa 67 wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa (UNBoA), Jumanne, 23 Julai, 2013 mjini New York, Marekani.

Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa saini ripoti 15 zilizoidhinishwa. Kutoka kushoto walioketi ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania),Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China) na Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza).

Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa (UNBoA) wakiwa katika picha ya pamoja. Kuanzania kushoto ni Bw. Ludovick S. L. Utouh (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania), Bw. Amnyas Morse (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Uingereza) na Bw. Lui Jiayi (Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China).

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bw. Ludovick S. L. Utouh (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Hellen Clark Mtendaji Mkuu wa UNDP (wapili kushoto) baada ya mazungumzo ya pamoja na menejimenti ya shirika hilo.