
TAARIFA ambazo zimetumwa na mmoja wa mashuda, kutokea Zanzibar, anasema ajali nyingine ya gari imetokea na watu watatu wamekufa papo hapo kati ya wananchi ambao wanaelekea eneo la Nungwi kuangalia ndugu zao waliopata ajali kwenye Meli ya Spice Islanders.
Na taarifa za sasa zinaeleza, watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na Vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kasi za Zanzibar ambazo ilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.
Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwanja vya Maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwa sasa Serikali inasafirisha maiti zote na majeruhi kuelekea Uwanja wa Maisara mjini, hivyo ndugu, jamaa na marafiki wasiendelee kwenda eneo la tukio Nungwi.
Poleni wafiwa huu ni msiba wa taifa mungu tupe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
Poleni sn! Inasikitisha.
Tupowe watu wa Zanzibar na watanzania kiujumla juu ya msiba huu wa kitaifa, poleni wafiwa naiyo kazi ya Allah, Mungu aziweke roho za marehemu pahala pema peponi, Amiin
Mie ni mzanzibar ambaye kwasasa niko shinyanga mgodini na haturuhusiwi kuingia sim, naomba taarifa yoyote itakayojiri mniarifu kupitia email yangu, niko field
Ok, jitahidi tu kutembelea mtandao huu tutatoa taarifa yote.
mbona siamini kama hiyo picha ni yakikweli au bado unatumia picha nyengine ambazo hazihusiki.mimi ni mmoja ambae alihudhuria katika tukio hilo na hivi sasa nipo maisara kusikiliza idadi ya watu ni wangapi lakin bado hakuna lolote linaloendelea isipokua blablaa tu.Je unashindwa kusema ni abiria wangapi ambao wakuemo katika meli hiyo?mimi naweza kusema kwani najua meli za pemba zinavyo sheheni abiria na mizigo.
Nikweli kwamba ni ajali mbaya sana amboyo imetokea katika bandari yetu lakini bado wananchi wanahamu yakujua ni abiria wangapi ambao walikuemo katika meli hiyo bado kuna utata mkubwa katika familia mbalimbali juu ya ajali hiyo.Tumepata kujua idadi ndogo(250) ya watu ambao wameokolewa lakin bado mamia ya abiria yapo katika kina cha maji.Je ni watu wangapi ambao wameshapoteza maisha yao kiukweli bado hali ni mbaya sana hapa zanziibar kama watu waliookolewa ni hao basi kuna 350 bado wapo katika maafa haya bado tunahitaji msada wa hali ya juu.
R.I.P
bado nipo katika viwanja vya maisara ambapo mamia ya wananchi wanashuhudia na kuziangali maiti ambazo zinapitishwa na ambao wameokolewa lakini bado serikali hajatoa idadi kamili nii abiri wangapi waliokuemo katika meli hiyo.nimezungumza na mmoja kati ya waliokua wanaokoa watu katika ajali hiyo “bado hali ni mbaya sana kwani bado watu ni wengi sana ambao hajaokolewa katika ajali hiyo japokua serikali inasema imefanikiwa kuokoa lakini bado hali mbaya”
polen ndugu zangu.2po pamoja
Poleni sana ndugu zetu kwa ajali ya basi na ya gari
POLENI MNO KWA AJALI YA MELI
Poleni sana majeruhi, na wafiwa wote. Mungu azidi kuwapa faraja.
poleni ndugu zetu wazanzibar tuko pamoja, Mungu awatie nguvu katika tukio hilo
poleni jamani
Kwa kweli inasikitisha sana kwa kutokea ajali za mara kwa mara hapa tanzania. Tunasikitika sana kwa kupoteza ndugu zetu, marafiki zetu, watoto wetu, baba na mama zetu katika ajali za kizembe ambazo zaweza kuepukika. Hasa kinachonipa hasira zaidi ni kwa nini vyombo hivi havikaguliwi mara kwa mara na mamlaka husika? au ndo kusema wameajiriwa kukaa ofisini kwa kupiga soga na kusoma magazeti? Jamani innaniuma sana.
poleni sana wafiwa, Mwenyezi Mungu awatie nguvu na hekma na busara katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.
Jina la Bwana lihimidiwe.
Beda S. Msacky
Nawapa pole sana wazanziber,msiba ni wetu wote. Allah awafanyie wepesi waliotangulia mbele ya haki,
Poleni sana ndugu zangu kwa msiba mkubwa uliotupata
Poleni sana wafiwa,majeruhi na mlionusurika MUNGU AWAJAZE UVUMILIVU
POLENI SANA ZANZIBAR NA TANZANIA WOTE KWA UJUMLA, ROHO ZA MAREHEMU WAPATE REHEMA KWA MUNGU WAPUMZIKE KWA AMANI, Amen
POLENI SANA ZANZIBAR NA TANZANIA KWA UJUMLA, ROHO ZA MAREHEMU WAPATE REHEMA KWA MUNGU WAPUMZIKE KWA AMANI, Amen
R.I.P