








NMB Yadhamini Wiki ya Uwekezaji Ziwa Tanganyika Sumbawanga
NMB imedhamini wiki ya uwekezaji ukanda wa ziwa Tanganyika-Mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi lenye lengo la kuvutia uwekezaji katika kanda hii. Katika wiki ya uwekezaji inayofikia tamati tarehe 2 Novemba 2014, NMB imedhamini shughuli zote kwa kuanzia maonyesho ya wajasiliamali (SIDO), uzinduzi wa wilaya ya Kalambo ambayo inategemewa kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete, na kongamano lenyewe ambalo linaratibiwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya chini ya mgeni rasmi ambaye ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais pia anatarajiwa kufungua jengo la kisasa la NMB Sumbawanga Novemba Mosi, 2014. Katika wiki hii, pia NMB pia imetoa madawati yenye thamani ya Shilingi Milion 5 kwa Shule ya sekondari Msakila ya mjini Sumbawanga na Vifaa vya hospitali vya Shilingi Milioni 5 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa Mjini Sumbawanga.
