Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ifunda mkoani Iringa, ambapo CCM ilizindua rasmi kampeni katika jimbo la Kalenga wakimnadi mgombea wao kwa tiketi ya chama hicho Bw. Godfrey Mgimwa na kuwaasa wanakalenga kumchagua Godfrey Mgimwa kwani ni mwakilishi wao kamili kutokana na kwamba ilani inayotekelezwa mpaka mwaka 2015 ni ya Cmaha cha Mapinduzi hivyo Mgimwa ataisimamia vyema na kukimalizia kipindi cha miezi ishirini iliyobaki kwa maendeleo ya wanakalenga.