
Huku kwetu Kata ya Kirando, wilayani Nkasi Bucha kuandikwa hivi sio tatizo, kwa kuwa tunakubaliana na kuvumiliana…! Pichani ni moja ya bucha linalochinja nyama kwaajili ya wakristu.

Uhamasishaji utamaduni wa kunawa mikono kwa afya, pichani ni eneo maalumu la kuosha mikono mara baada ya shughuli anuai zinazo iacha mikono si salama kiusafi. Hapa ni Katika moja ya Shule za Sekondari Kirando.

Pichani juu ni baadhi ya maboti yanayotumika kusafairisha abiria kutoka Kata ya Kirando, Nkasi kwenda vijiji vya jirani Ziwa Tanganyika

Usione udogo wa boti hili maalumu kwa kubeba mizigo lina uwezo wa kubeba gunia 1000 za bidhaa anuai…!

Mwandishi wa mtandao wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kulia) akizungumza na mmoja wa wadau wa usafirishaji abiria alipokuwa katika ziara ya kutembelea vijiji kadhaa vya Wilaya ya Nkasi, Rukwa.

Mwandishi wa dev.kisakuzi.com akiangalia kimea cha mahindi ambacho hutumika kutengenezea pombe aina ya komoni moja ya vijiji vya Nkasi.