
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiongea na washindi wa tiketi za VIP kutoka kote nchini (hawapo pichani) baada ya washindi hao kuwasili kwa ajili ya ziara kiwandani hapo, washindi hao
watashuhudia tamasha la Serengeti Fiesta kesho jijini Dr es Salaam.
Baadhi ya washindi wa tiketi za VIP wakipata picha ya pamoja katika kiwanda cha bia cha Serengeti. .
Meneja wa mipango kwa wateja wa kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela akiwakaribisha washindi wa tiketi za VIP (hawapo pichani) baada ya washindi hao kutembelea kiwanda cha bia cha Serengeti. washindi wa VIP 75 watanufaika na ushindi huo kwa siku nne hapa jijini Dar es salaam.
Maandalizi ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ambalo litafanyika hapo baadaye viwanja vya Leaders Club.
Baadhi ya mafundi wakifunga TV zitakazokuwa zikirusha matukio na matangazo anuai ndani ya tamasha hilo.
Ni katika viwanja vya Leaders Club ambapo shamrashamra na maandalizi ya steji pamoja na kuandaa mazingira kwa ajili ya tamasha la Serengeti Fiesta ambalo litafanyika baadaye kidogo.