TSh bilioni 4.46 Kukamilisha Mradi wa Umeme Kigoma.

Na Immaculate Makilika- Dodoma

SERIKALI imedhamiria kutafuta fedha kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na nje ya nchi ikiwemo washirika mbalimabli wa maendeleo ili kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa kupeleka umeme Kigoma.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene alipokuwa akijibu swali ya David Kafulila Mbunge wa (Kigoma Kusini-CHADEMA) yaliyouliza je, ni lini ujenzi wa mradi wa umeme wa Malagarasi utaanza ambapo ‘study ya Igamba III’ imekamilika na kuonesha tutaweza kupata zaidi ya MW 43,na je Serikali haioni busara kuzungumza na mifuko ya hifadhi za jamii ili wawekeze kwenye mradi huo.

Na swali lingine likiuliza ni lini Serikali itaanza utekelezaji ahadi yake ya kutumia umeme unaopatikana Kigoma mjini kufikishwa Makao Makuu ya uvinza kama ilivyotakiwa kisera.

Wakati Naibu Waziri alipokuwa akijibu maswali hayo leo Bungeni Dodoma alisema kwamba ,Mkataba wa ufadhili wa Millenium Challenge Corporation(MCC) kwa maradi wa umeme wa maji wa Malagarasi III MW 44.8(Malagarasi stage III 44.8 MW Hydro Power Plant) ilikuwa ni ‘ Feasibility study ‘tu na sio zaidi ya hapo.

Hata hivyo alisema utekelezaji wa mradi huo unategemea na upatikanaji wa fedha.

Aidha Serikali inatarajia kutumia umeme unaozalishwa na generator ya Mafuta ya Diesel/Kigoma Mjini na kuunganisha Makao Makuu ya Wilaya ya Uvinza kupitia mapango kabambe wa Umeme vijiini awamu ya pili chini ya ya uwezeshaji wa wakala wa Nishati vijijini (REA)

Kazi ya kupeleka umeme Makao Makuu ya Wilaya ya Uvinza itajumuisha ujenzi wa njia za umemem,ufungaji wa transfoma na kuwaunganisha wateja wa awali 2,100 .Gharama ya mradi huo inakadiriwa kua sh bilioni 4.46.