
Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (mwenye blauzi ya kijani) na Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Julius Mogore (mbele) wakiongoza shughuli za usafi kuzunguka maeneo ya Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 1, 2013 katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika. Siku hiyo itaadhimishwa kitaifa siku ya Jumapili.