
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na mkewe Bi. Yasim Davutoglu wakiwagawia zawadi watoto wanaolelewa katika kituo cha CHAKUWAMA Sinza jijini Dar es Salaam walipotembelea kituo hicho hapo jana.

Akiongea na vyombo vya habari Balozi wa Uturuki nchini Mh. Ali Davutoglu kuhusu maonesho ya mitindo kwaajili ya kucangia ujenzi wa kituo cha CHAKUWAMA yatakayofanyika Jumamosi trh 08/12/2012, Serena Hoteli jijini Dar es Salaam. Katikati ni Bi Yasim(mke wa balozi wa uturuki) akiwa amembeba mwanae anayemlea katika kituo hicho na kulia kwake ni Katibu wa kituo cha CHAKUWAMA Hassan Hamisi.