
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya. Picha na Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi cha Kenya (National Defence College) kilichoko Karen, Nairobi, na baadaye kupiga picha ya pamoja na ujumbe wake, wanachuo na viongzozi wa chuo hicho. Picha na Ikulu

Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.