Mchezaji Patrick Mafisango wa Simba afariki dunia

Mchezaji wa kimataifa Patrick Mafisango wa Simba SC

MCHEZAJI Patrick Mafisango wa timu ya Simba ya Dar es Salaam amefariki dunia leo kwa ajali ya gari katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Taarifa ambazo zimetolewa kutoka Klabu ya Simba zimesema Mafisango amefariki dunia leo asubuhi kwa ajali ya gari maeneo ya Tazara. Mtandao huu utawaletea taarifa zaidi za tukio hilo muda mfupi baadaye. Mtandao huu pia unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na klabu nzima ya Simba kwa pigo hilo.

Related Post

6 thoughts on “Mchezaji Patrick Mafisango wa Simba afariki dunia

  1. Daah wanasimba tutmkumbuka jaama msimu huu alikuwa kwenye kiwango cha juu sana…Mungu ailazi roho ya marehemu mahala pema…

  2. tunamshukuru Mungu kwa kipindi tulichokuwa na Patrick,japokuwa mchango wake ulikuwa bado unahitajika lakini tunaamini aliyemchukua kampenda zaidi.

    tuyaenzi mema yote aliyotuachia kwa ustawi wa jamii yetu.

    mungu ailaze mahali pema Patrick

    1. Nami nahuzunika kwa kusikia tukio la ajali ya mwanasport wetu, kufa kupo na wote tutakufa,tuwe tayari na tuone ni kawaida tu ya msiba kama miingine sema tu yeye ni maarufu kwa kutangazwa.

Comments are closed.