Waziri Mkuu Pinda kumwakilisha Rais Kikwete Angola

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda anaondoka Dar es Salaam leo, Alhamisi ya Mei 31, 2012 kwenda Luanda, Angola kuhudhuria kikao cha Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu, Pinda anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye leo anatarajiwa kufungua mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) huko Arusha.

Mara baada ya kuwasili, leo jioni Waziri Mkuu atahudhuria kikao cha TROIKA ambacho kinajumuisha Wakuu wa Nchi kitakachofanyika Ikulu ya nchi hiyo na usiku atashiriki hafla maalum iliyoandaliwa kwa viongozi wakuu wa nchi za SADC.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi za SADC ambao umepangwa kufanyika Juni Mosi, 2012, utatanguliwa na mkutano wa mawaziri unaoanza Mei 31, 2012 chini ya uenyekiti wa Waziri ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini nchini kesho kutwa (Jumamosi, Juni 2, 2012).

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.