Wapinzani Misri Wagomea Mazungumzo, Rais Atangaza Hali ya Hatari

Rais wa Misri, Mohammed Morsy
Rais wa Misri, Mohammed Morsy

KUNDI kubwa la upinzani nchini Misri limesema halitahudhuria mazungumzo yanayoandaliwa na Rais Mohamed Morsi hadi pale masharti yatakapotimizwa. Mkutano huo ulipanga kumaliza machafuko ambayo yamekuwa yakiendelea katika miji kadhaa katika siku za hivi karibuni.

Awali Rais Morsey alitangaza hali ya hatari ya muda wa mwezi mzima katika miji ya Port Said, Suez na Ismailiya kufuatia siku kadhaa ya maandamano na fujo.

Alisema kuwa pia ameweka amri ya kutotoka nje usiku kucha. Kiongozi wa kundi la upinzani la Free Egyptians Party, Dr Ahmed Saeed, ameaimbia BBC kuwa rais Mosri anapaswa kufanya juhudi zaidi kurejesha imani ya wananchi. Rais wa Misri Mohammed Morsi ametangaza hali ya tahadhari katika miji ya Port Said, Suez na Ismalia baada ya siku kadhaa za machafuko makali.

“Kuanzia Jumatatu na kwa siku 30 zijazo watu hawaruhusiwi kutoka nje baada ya saa 12 hadi asubuhi,” alisema alipo lihutubia taifa. “Huwa kwa kawaida napinga hali za tahadhari, lakini ilibidi niwalinde wananchi na kukomesha umwagikaji damu basi ikanabidi nifanye hivyo,” rais alisema.

Takriban watu 33 people walikufa mnamo wikiendi huko Port Said, ambapo uamuzi wa mahakama ulisababisha vurugu kuzuka. Kutoridhika na uongozi wa Bwana Morsi’s kulizua fujo kwingine nchini.

Katika mji mkuu wa Cairo, waadamanaji wailokuwa wanaipinga serikali walipambana na vikosi vya ulinzi karibu Uwanja wa Tahrir kwa siku ya nne mfululizo.
Upinzani

Upinzani unamlaumu Morsi kwa kutawala kimabavu na kuipa kipaumbele katiba mpya ambayo hailindi kikamilfu haki za kuabudu wala za maoni. Serikali pia imelaumiwa kwa kutodhibiti hali ya uchumi, inayozidi kuzorota. Bwana Morsi alisema kwamba angechukua hatua zaidi “kwa ajili ya Misri” na kwamba ilikuwa “wajibu wake” kama rais kufanya hivyo.

Aidha, aliwaalika viongozi wa kisiasa wakutane “katika majadiliano ya kitaifa ” mnamo Jumatatu. Ingawaje muungano mkubwa zaidi wa vyama pinzani nchini Misri, National Salvation Front, uliuunga mkono mualiko huo, ulilaumu sera za Morsi kwa kuzua vurugu.

Vurugu zilizuka Port Said baada ya mahakama kuwahukumu watu 21 kifo kwa kuhusika na fujo baada ya mechi ya kandanda Februari 2012.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.