Wanafunzi Dar Waadhimisha Valentine Day kwa Mtazamo wa Kijinsia

Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia.
Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia.

Na Thehabari.com

WANAFUNZI mbalimbali kutoka katika baadhi ya shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo wameadhimisha Siku Kuu ya Wapendanao (Valentine Day) kwa mtanzamo wa Kijinsia ikiwa ni
kushinikiza jamii kuadhimisha sherehe hiyo kwa mtazamo tofauti na mazoea kwa siku hiyo.

Wakizungumza katika maadhimisho hayo wengi waliitaka jamii kubadili mtazamo wa maadhimisho ya Valentine na kuijali jamii zaidi isiojiweza kwa kuisaidia kuonesha upendo na kuacha kuegemea katika mapenzi ambayo yamekuwa yakiipotosha jamii.

Mwanafunzi Grace David kutoka Shule ya Sekondari Loyola alisema mapenzi ya kweli hayawezi kuoneshwa kwa mtu kwa siku moja pekee, bali hali hiyo inapaswa kuwepo siku zote tofauti na mtazamo ya vijana wengi wanavyoichukulia ‘Valentine Day’.

Naye Meneja wa Idara ya Habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na wanafunzi alisema siku ya Valentine hivi sasa imegeuzwa kibiashara zaidi na jamii kiasi cha kuyaathiri makundi mengine ya jamii kwa namna mbalimbali.

Alisema takwimu zinaonesha kuwa kadi za ujumbe wa mapenzi zinauzwa kwa kiasi kikubwa siku hiyo ukilinganisha na sikuu kuu zingine, huku biashara nyingine za starehe zikifanywa kiasi kikubwa.

Alisema jamii ina kila sababu ya kuanza kubadilika na kuadhimisha siku hiyo kwa kujitolea kwa makundi yasiojiweza kama watoto yatima, wazee na wajane ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Hata hivyo alisema ukatili wa kijinsia na mapenzi umekuwa ukiibuka kwa kasi katika siku kuu hiyo; kama wapenzi (katika ndoa) kuwasaliti wapendwa wao, ukatili wa kimapenzi, vipingo na starehe zisizo na tija jambo ambalo linafanya makundi yasio na uwezo kutengwa.

Aidha aliongeza kuwa wanafunzi nao wamekuwa wakijikuta wakitoka katika maadili yao na kujiingiza katika mapenzi na ngono zembe jambo ambalo limekuwa likiwaathiri kwa kiasi kikubwa.

“Valentine ni maadhimisho ya kumbukumbu ya mwanaharakati aliyekuwa mtetezi wa haki za makundi ya vijana katika jamii ya Ki-nubi ambao walinyimwa haki zao katika masuala ya mahusiano, sasa tunaisherekea kimapenzi zaidi…,” alisema Bi. Liundi.

Makundi hayo ya wanafunzi kutoka shule za Sekondari Yusuf Makamba, Loyola (Loyola High School), Mabibo, Perfect Vision na Sinza Tower yamekutanishwa na TGNP kwa kushirikiana na Taasisi ya Soma Book Cafe ya jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya maadhimidho hayo ni “Wantanzania Tupendane Bila Aina Yoyote ya Unyonyaji, Ubaguzi na Ukatili wa Kijinsia”

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sinza Tower wakifanya maigizo kuonesha madhara ya wanafunzi kujihusisha na mapenzi wawapo shuleni.

 

Msimulizi wa Hadithi za fasihi, Rupal
Ganatra (kulia) akitoa simulizi kwa wanafunzi walioshiriki katika
Maadhimisho ya Siku ya Wapendao kwa Mrengo wa Kijinsia katika bustani ya SOMA.

 

Meneja wa Idara ya Habari na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi (katikati) akifuatilia maigizo ya wanafunzi katika hafla hiyo.

 

Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi (aliyeshika kipaza sauti) akiimba na wanafunzi (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa walioshiriki Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia Dar es Salaam.

 

Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi (kulia) akizungumza na wanafunzi anuai waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Valentine kwa Mrengo wa Kijinsia.

 

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Yusuf Makamba wakiwasilisha igizo lao katika hafla hiyo. Pichani aliyepiga magoti ni msichana aliyejiingiza kwenye mapenzi shuleni na kujikuta akipata ujauzito ambao ulikataliwa na aliyempa ujauzito huo (kijana anayeonekana kumuomba)-hili ni igizo tu.

 

Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho hayo.

 

Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.

 

Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.

 

Vikundi vya wanafunzi wakiwa katika majadiliano na tafakari baada ya kuwasilishwa kwa mada mbalimbali katika hafla hiyo.

 

Kutoka kushoto ni Lilian K, Lilian Liundi na Deo Temba wote kutoka Idara ya Habari ya Mtandao wa Jinsia Tanzaniua (TGNP) wakijadiliana jambo kwenye maadhimisho ya Siku ya Wapendanao kwa Mrengo wa Kijinsia.

 

Wanafunzi wakiwa katika majadiliano kwenye vikundi. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Habari TGNP, Lilian Liundi akiwasikiliza.

 

 

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.