Waliokufa na Mv. SKAGIT Zanzibar waombewa

Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, (wa tano kushoto) pamja na Viongozi wengine wa Serikali wakiungana na Waislamu katika Swala ya kuwaombea Dua Abiria waliofariki katika Ajali ya Meli Mv Skagit ya Kampuni ya Seagul, iliyozama hivikaribuni ikitokea Dar es Salaam kuelekea Zanzibar, swala hiyo ikiongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh
Saleh Omar Kabi, katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, leo ameungana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa katika dua maalum ya hitma pamoja na Sala maalum ya Maiti (Salatul Mayyit al-ghaib), iliyosomwa huko katika msikiti Mushawar, Mwembeshauri mjini Zanzibar.

Sala na dua hiyo ni maalum kwa ajili ya kuwaombea watu waliokufa kutokana na ajali ya kuzama kwa meli ya MV SKAGIT, iliyotokea hivi karibuni wakati meli hiyo ilipokuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kuja Zanzibar na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa

Katika sala na dua hiyo viongozi mbali mbali wa dini, vyama na Serikali walihudhuria akiwemo Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Dk. Mohammed Kharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais mstaafu wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Khabh, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Spika wa Baraza la Wawakishi Pandu Ameir Kificho, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Abdalla Mwinyi Khamis, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wabunge, Wawakilishi, Mashekhe mbali mbali wa Zanzibar na Tanzania Bara pamoja na wananchi na viongozi wengine.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.