Waliochaguliwa kufanya usaili Jeshi la Polisi hadharani

Na Mwandishi Wetu, Musoma

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limetoa majina ya vijana ambao wamechaguliwa kwa ajili ya kufanya usaili wa kujiunga na jeshi hilo ambapo kanda ya ziwa utafanyika Julai 2 hadi 4 mwaka huu katika ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Absalom Mwakyoma alisema kuwa majina hayo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo zilizopo katika ofisi za Mkoa na wilaya zote.

“Mwaka huu tumeamua kuchukua vijana watakaojiunga na jeshi letu kutoka mashuleni ambao wamemaliza kidato cha nne mwaka jana na cha sita mwaka huu hivyo tunawaamba vijana wote waende wasome na wajue kama jina lake lipo katika orodha yetu,”

“Hii tumerahisisha ili kupunguza msongamano wa vijana kufika katika ofisi zetu na kuulizia ajira hizo na kama unatumia mtandao tafuta katika mtandao wetu wa www.policeforce.go.tz na utaona jina lako na vituo vya usaili,”alisema.

Alisema kuwa vijana ambao wataona majina yao waende katika kituo cha usaili katika kanda mbalimbali kama zitavyoonesha katika matangazo yao wakiwa na vyeti halisi vya masoma yake na cheti cha kuzaliwa.

“Tunasisitiza kwa watahiniwa kufika katika vituo hivyo na vyeti vyao pia tunawakumbusha kuwa hati ya kiapo ya mahakamani haitakubaliwa na awe na barua ya wadhamini wawili wanaomfahamu vizuri zinazoelezea mahusiano baina yao na muombaji na namba za simu na anuani halisi ambazo zinatumika,”alisema Kamanda Mwakyoma.

Alisema kuwa kila kijana ambaye ataona jina lake atajigharamia gharama zote za usafiri, chakula na malazi muda wote wa usaili pamoja na kalamu za wino kwa ajili ya kuandikia.

Kamanda Mwakyoma alisema kuwa mtahiniwa anaruhusiwa kufanya usaili katika kanda yoyote kulingana na tarehe husika kuepusha usumbufu wa kusafiri safari ya mbali.

Jeshi hilo la Polisi limeamua kutumia mfumo huo ambao ulikuwa unatumika miaka ya nyuma walikuwa wanatoa moja kwa moja mashuleni ili kuepusha upendeleo na malalamiko kwa wanyonge.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Related posts

11 Comments

 1. Joseph tibesigwa

  I am a Tanzanian citizen bt studied in kenya thus aquiring kenyan certificates,does that hinder me from joining the police force?

  Reply
 2. jenipha.k.sitephano

  naitwa jenipha k. sitephano nilikuanaomba na fasi ya kujiunga na jeshi la police TANZANIA kwa lengo la kuitumikia nchi yangu nitafurai kama ombilangu lita kubaliwa ni muitimu wa kidato cha nne 2016 nitashukulu kama nitakubaliwa na ipenda nchi yangu sana

  Reply
 3. jenipha.k.sitephano

  naitwa jenipha.k.sitephano nimuitimu wa kidato cha nne 2016nilikua naomba nafasi ya kujiunga na jesh la police TANZANIA ninaipenda sana kazi ya upolie nitafurai kama maombi yangu yata kubaliwa natakia kaz njema

  Reply
 4. Patrick Kessy

  Comment…Mimi naitwa Patrick Kessy. nimemaliza kidato cha NNE mwaka 2016. ninapenda saana kazi ya polisi kutumikia taifa langu kwa nguvu zangu zote…Napenda saana taifa language.. naomba kujiunga na jeshi la police Tanzania

  Reply
 5. Patrick Kessy

  Comment…naombeni nafasi ya kujiunga na jeshi LA Polisi naahidi kutumia nafasi hiyo kama inavyohitajika na kuheshimu mafunzo na kujituma ili kuwa Polisi mwenye maadili bila kukiunga maadili ya kazi, mafunzo na wala kukiuka maagizo ya Amiri jeshi mkuu na viongoz wengine naaomba nafasi hiyo ya kuitumikia nchi yangu ya Tanzania

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published.