SYRIA: vita vya wenyewe kwa wenyewe vyanukia

mjumbe wa UN na Arab league nchini Syria Kofi Annan
mjumbe wa UN na Arab league nchini Syria Kofi Annan

MKUU wa ujumbe wa umoja wa mataifa ameonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe Syria baada ya wachunguzi hao kuhesabu miili 92, 32 ikiwa ni ya watoto ,katikati ya mji wa Houla kufuatia ripoti za mauaji.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amejiunga na sauti za kimataifa kushutumu mauaji hayo siku ya Jumamosi , huku kukiwa na miito kwa dunia kuchukua hatua kusitisha umwagikaji wa damu.
Jeshi la waasi la Free Syria, Syria huru , FSA, limesema halifuati tena mpango unaoungwa mkono na umoja wa mataifa nchini Syria hadi pale kutakapokuwa na uingilia kati wa umoja wa mataifa kuzuwia mauaji ya raia, na kutoa wito wa mashambulio ya anga dhidi ya majeshi ya serikali.
Mkuu wa ujumbe wa umoja wa mataifa meja jenerali Robert Mood amekiita kile kilichotokea mjini Houla , kuwa maafa ya kinyama. Wachunguzi wa kiraia na kijeshi wa Umoja wa mataifa walikwenda mjini Houla na kuhesabu miili 32 ya watoto na zaidi ya 60 ya watu wazima waliouwawa, Mood amewaambia waandishi habari mjini Damascus siku ya Jumamosi.
Kundi linalochunguza hali nchini Syria limesema kuwa watu 114 wameuwawa katika mji wa Houla. Yeyote alieanzisha, yeyote anayehusika na yeyote aliyefanya vitendo hivyo vya kuchukiza anapaswa kuwajibishwa, amesema Mood.
Wale wanaotumia nguvu kwa ajili ya kutimiza ajenda zao wataleta hali ya kutokuwa thabiti zaidi, hali ambayo haitabiriki na huenda ikaelekeza nchi hiyo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, ameongeka mkuu huyo wa ujumbe wa umoja wa mataifa.
Ban Ki-moon na Kofi Annan ambaye ni mjumbe wa umoja wa mataifa na mataifa ya umoja wa mataifa ya kiarabu , Arab League, ambaye amekuwa mpatanishi wa makubaliano ya kusitisha mapigano, ambayo yamekuwa yakikiukwa kila siku tangu yalipoanza kufanyakazi Aprili 12, wamesema kuwa mauaji hayo ya kinyama yanakiuka sheria za kimataifa.
Uhalifu huu wa kinyama na unaochukiza , uliowahusisha matumizi bila kujali na ya kupita kiasi ya nguvu , ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa, msemaji wa umoja wa mataifa amemnukuu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon akisema.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton pia ameshutumu vikali , mauaji hayo na kusema Marekani itafanyakazi pamoja na washirika wake wa kimataifa kuongeza mbinyo dhidi ya rais Bashar al-Assad na washirika wake.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Hillary Rodham Clinton
Utawala unaohusisha mauaji na hofu ili kuwatawala raia wake ni lazima ufikie mwisho, ameongeza. Shutuma pia zimemiminika kutoka umoja wa Ulaya. Uingereza, Ufaransa na Ujerumani , huku waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akisema kuwa anafanya matayarisho ya mkutano wa marafiki wa Syria.
Mwenzake wa Uingereza William Hague amesema , “tutatoa wito wa kufanyika kioa cha dharura cha baraza la usalama la umoja wa mataifa katika siku za hivi karibuni.”
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema ameshtushwa na kuchukizwa na mauaji hayo.
Meja jenerali Mood amethibitisha kuwa makombora na vifaru viliishambulia mji wa Houla na kutoa wito kwa serikali ya Syria kuacha kutumia silaha kali na kwa makundi yote kusitisha matumizi ya nguvu kwa aina yoyote ile iwayo.

-DW

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.