Sekretarieti ya CCM Taifa Yakagua Daraja Malagarasi

KINANA AKIHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA NGURUKA UVINZA MKOANI KIGOMA JANUARI 28, 2013

KINANA AKIHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA NGURUKA UVINZA MKOANI KIGOMA JANUARI 28, 2013
NAPE AKIZUNGUMZA NGURUKA KWENYE MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KWENYE UWANJA WA SHULE YA MSINGI, NGURUKA MKOANI KIGOMA
Nape akishiriki kupiga ngoma ya kuongoza matembezi kuingia mji mdogo wa Nguruka, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, kwenda kwenye mkuytano wa hadhara wa CCM, Nguruka, Januari 28, 2013. Pembeni yake ni Asha Baraka
Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Sik You, (wapili kushoto) akimtembeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watatu kushoto) na ujumbe wake kushuhudia hali ya ujenzi wa daraja hilo ilivyo, Januari 28, 2013, wilayani Uvinza mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa You mradi huo umekamilika kwa asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika Aprili mwaka huu. Wengine ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (wanne) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wapili kushoto) . Kinana na ujumbe wake wapo mkoani Kigoma kwa ajili ya kushiriki kwenye kilele cha sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Januari 3, 2013. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).
Kinana akizungumza na mwananchi wa Kigoma Amani Khalidi wakati akikagua ujenzi wa daraja la Malagarasi. kuhsoto ni Meneja mradi wa ujenzi daraja la Malagarasi wa Kampuni ya Korea ya Hanil, Jung Yong

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.