Rais wa Ghana John Attah Mills afariki

john-atta-mills


Rais wa Ghana John Atta Mills amefariki ghafla wakati akipata matibabu.
Taarifa kutoka Ofisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng’ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
” Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito… Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana ” taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.

-BBC

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.