Rais Kikwete apokea hati za mabalozi

Rais Kikwete apokea hati za mabalozi

RAIS Jakaya Kikwete leo Ikulu ya Dar es Salaam, amepokea Hati za Utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa Ujerumani Bwana Klaus-Dieter Brandes na kuagana na balozi wa Saudi Arabia anaemaliza muda wake hapa nchini Ali Abdulla Al Jarbou.
Mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho Rais amefanya mazungumzo na balozi Brandes na kumwambia Tanzania inashukuru kwa misaada thabiti ya Ujerumani hapa nchini katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, maji, Afya, mazingira na uchumi.
Naye balozi Brandes amemhakikishia Rais Kikwete kuwa atashirikiana na Serikali ya Tanzania kwa karibu na kusimamia misaada zaidi katika vipaumbele vya serikali.
Kabla ya kuhamishia kituo chake cha kazi hapa Dar-es-Salaam, balozi Brandes alikuwa Abu Dhabi na Umoja wa nchi za Kiarabu.
Mapema katika mazungumzo yake na balozi Al Jarbou, Rais ameishukuru Saudi Arabia kwa ushirikiano mkubwa alioutoa balozi katika kipindi chake chote cha miaka minne alichokuwa hapa nchini na amemtakia Balozi huyo kila la kheri katika shughuli zake zingine ambazo atapangiwa mara baada ya kurudi nchini mwake.

Related Post

One thought on “Rais Kikwete apokea hati za mabalozi

  1. Superb blog you have here but I was wondering if you knew of any message boards that cover the same topics talked about in this article? I’d really love to be a part of community where I can get feed-back from other knowledgeable individuals that share the same interest. If you have any suggestions, please let me know. Cheers!

Comments are closed.