Maofisa wastaafu wa JWTZ waagwa Dar es Salaam



Maafisa wa Jeshi la wananchi wa Tanzania Jeshi la Kujenga Taifa wakiwasukuma gari maalum kwa ajili Mameja Jenerali wastaafu wa Jeshi hilo mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga jana katika Kambi ya Abdallah Twalipo jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali (mstaafu) Yodan Mtaluma Koyi na Meja Jenerali(mstaafu) Salim Suleiman.


Mkuu wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Kujenga Taifa Jenerali Davis Mwamunyange (katikati) akiongea na waandishi wa habari jana katika kambi ya Abdallah Twalipo jijini Dar es salaam mara baada ya gwaride rasmi la kuwaaga Mameja Jenerali na Brigedia Jenerali waliostaafu. (Picha zote na Vicent Tiganya-Maelezo, Dar es Salaam)

Related Post

One thought on “Maofisa wastaafu wa JWTZ waagwa Dar es Salaam

  1. Kazi nzuri na yakutukuka mliyo lifanyia taifa hongereni ila kwa niaba ya wananchi tunawaomba sana tumieni busara zenu kulikosoa Jeshi letu pale litakapo onekana kukiuka maadili hususani linapoingia katika migogoro na wanajamii wakati mwingine kwa maslahi binafsi ya afisa mmoja mmoja na wakati mwingine kwa jamii kwa ujumla mabavu si suluhisho pekee la kutatua migogoro.Jeshi limejipatia heshima kubwa tokea Uhuru wa Taifa hili hadi hapa tulipo lakini wasi wasi wangu upo kwa baadhi ya wanajeshi wanaotumia nyadhifa zao vibaya na kuwanyanyasa baadhi ya raia.Mimi binafsi niliwahi kuingia katika mgogoro na askari wa JWTZ kilichosaidia nimekomboka kifikra nilishindana naye kwa hoja hadi Upanga na yalikwisha na kwa sasa ni swahiba wangu mkubwa lakini si achi kuishi kwa tahadhari kwani nawajua vema.Je kwa mtanzania wakawaida asiyejua haki zake za msingi atakuwa katika muktadha upi mliobaki litumikieni Taifa kwa nidhamu ya hali ya juu kwani adui zenu ni wavamizi wa mipaka yetu na wasio itakia mema inchi hii.Kwa namna ya Pekee nampongeza Mh Davis Mwamunyange kwa kazi nzuri na waambata wakijeshi wote bila kumsahau ndugu yangu Mze Shimbo Mhazini wa majeshi Tanzania.Mwisho sifa za pekee kwa The habari team be blessed.

Comments are closed.