Mambo Nane Yatakayokuongezea Furaha

1) Toa shukrani.

Kila siku ukiamka asubuhi Mshukuru Mungu kwa kukuwezesha kuamka salama na mwenye afya. Kitendo cha kushukuru kitakufanya ujione una jambo la kushukuru na kuwa wewe ni mwenye bahati. Kuna mambo mengi sana ya kushukuru, kama vile afya yako, nyumba unayolala, gari unaloendesha, chakula unachokula, mpenzi uliyenaye n.k. Fikiria mambo matano ya kushukuru kila siku asubuhi na utajiongezea furaha maishani mwako.

asante-sana

2) Amka mapema

Uchunguzi uliofanywa na chuo kikuu cha boston huko Marekani kinaonyesha kuwa watu wanaoamka mapema wanakuwa na furaha zaidi kuliko watu wanaochelewa sana kuamka. Kama unaweza ni vyema kuamka saa 11 au 12 asubuhi.

amka-mapema-asubuhi

3) Panga ratiba ya siku nzima

Umeshawahi kurudi nyumbani jioni na kujiona kama siku yako imepotea bure na hamna cha maana ulichokifanya? wakati mwingine inawezekana kabisa kuwa umefanya kazi nyingi lakini kwasababu hukupanga ni nini utafanya siku hiyo unajiona kuwa hujafanya chochote. Ni vyema kuandika list ya vitu unavyopanga siku nzima, mwisho wa siku ukifika unaangalia list ya vitu ulivyovifanya na kuvimaliza, utajipongeza na kulala vizuri ukijua siku yako imekuwa ya mafanikio.

4)Fanya mazoezi

Kufanya mazoezi kunasaidia kujisikia vizuri, kuwa na afya njema, kulala vizuri, kupendezesha ngozi na kujiepusha na magonjwa mbali mbali hasa yale yanayosababishwa na unene.

selteringelitedaily

5) Kula Breakfast

Kwa wale waliozoea kupiga desh asubuhi huu ndio muda muafaka kuacha hiyo tabia. Umeshasikia kuwa “breafast is the most important meal of the day”. Ukiacha tumbo bila chakula muda mrefu unajiweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Kumbuka wengi wetu huwa tunakula chakula cha jioni saa mbili usiku, ikifika saa mbili asubuhi tayari ni masaa 12 hujaweka kitu tumboni, ukipiga desh breakfast mpaka saa saba mchana hayo ni masaa 17 umekaa bila kuweka kitu tumboni. Faida nyingine ya kula breakfast ni kukupa nguvu na hujisikii umechoka choka ukifika kazini. Ukiona mtu ameingia kazini amenuna, muulize kama amekunywa chai na jibu lake litakuwa ni hapana.

20121007_121556

6) Mfanyie mtu yeyote jambo jema

kumfanyia mtu jambo jema inakufurahisha wewe na pia inamfurahisha mtu ambaye umemfanyia jambo jema, Na sio lazima huyo mtu awe ni ndugu yako au mtu aunayemjua. Mambo ya kufanya kumfurahisha mtu ni mengi sana, nitakupa mfano wa mambo machache ambayo mimi mwenyewe huwa nafanya. Mambo hayo ni kama kumfungulia mtu mlango, Kumsaidia omba omba barabarani, kumnunulia rafiki yako lunch, kumrushia bibi yako hela ya sukari, kumpa mtu lift ya gari n.k Hakikisha kila siku unamfanyia mtu jambo jema na itakuongezea wewe furaha.

7) Sikiliza muziki wenye furaha (up beat music)

Utakuta mtu anaingia kwenye gari asubuhi anaweka wimbo wa majonzi jinsi anavyo-m-miss bebi wake au nyimbo nyingine tu za huzuri, mwisho wake utaishia kujisikia mwenye huzuni. Sikiliza nyimbo zilizo changamka na utajisikia umechangamka na mwenye furaha.

8) Mpigia simu mtu na umwambie unampenda

Kusema neno nakupenda ni ngumu kidogo kwenye jamii yetu. Lakini jitahidi kusema nakupenda mara kwa mara, ukiongea na mke wako , mtoto wako, bibi yako waambie unawapenda. Kuna miujiza katika neno nakupenda na ukilitumia vizuri utaiona hiyo miujiza.

Je kuna jambo lolote ambalo wewe unafanya linakuongezea furaha..kama lipo acha comment hapo chini.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Related posts

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.