Kamati ya Miss Tanzania yawatembelea warembo Redds Miss Kurasini

Hashim Lundenga akizungumza na Warembo hao ikiwemo kuwasisitiza kuwa wajiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.
Hashim Lundenga akizungumza na Warembo hao ikiwemo kuwasisitiza kuwa wajiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.
Kamati hiyo pia ilihudhuria na Katibu Mkuu wake Bosco Majaliwa, Mkuu wa Itifaki, Albert Makoye, Ofisa Habari, Aidan Ricco na Ofisa wake Yason Mashaka.
Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Kurasini wakiwa katika Picha ya pamoja baada ya kuzungumza na Kamati ya Miss Tanzania.

Hashim Lundenga aliwataka warembo hao kujiheshimu maana urembo ni kazi kama zilivyo kazi nyingine na warembo wengi wanaojiheshimu na kuwa na tabia njema katika jamii huwa na mafanikio makubwa.

Wakati Nameems Wear wakiwa ni wadhamini wakuu, wakisaidiwa na Reds, Dodoma wine, Clouds FM, Lady Pepeta, Father Kidevu Blog, Jambo Leo, Aucland Tours & Safaris, Candy Bureau de Change, Flexip, PJ Amusement, Renzo Salon na Madishisha Video Production.

Aidha Jumla ya warembo 16 wamejitokeza kuwania taji la Redds Miss kurasini 2012, ambalo taji linashikiliwa na Top Model wa Miss Tanzania 2011, Mwajabu Juma.

Akiwataja warembo waliopo kambini na kunolewa na Mwajabu Juma akisaidiwa na Malkia wa vipaji wa Miss Tanzania 2011, Rose Hurbert ni Mariam Sadic (19), Johari Juma (20), Linda Deus (20), Irene Sostheness 20), Neemadoree Sylvery(29), Edna Magige (22), Lindanancy Joseph(20), Elizabeth Mkende (19), Betty Peter (22), Jennifer Njabili (18), Lilian Joseph (20), Farida Mrope (23),Christina Moses (20), Angle Gasper (19), Flaviana Maeda(22) na Sia Kimambo (19).

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.