Bungeni Dodoma Leo.

Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia habari  mbalimbali za magazeti yanayochapishwa kila siku nje ya ukumbi wa Bunge leo, Dodoma.

Wakuu wa mikoa na makatibu tawala kutoka mikoa mbalimbali nchini wakifuatilia kipindi cha Bunge cha maswali na majibu ya makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu leo mjini Dodoma.

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizungumza jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa akichangia bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya waziri leo. Pamoja na mambo mengine ameitaka serikali kufanya maamuzi magumu katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa maendeleo ya wananchi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge kutoka Dar es salaam nje ya ukumbi wa Bunge leo. Wanafunzi hao walikuwa bungeni Dodoma kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na Bunge kufuatia mwaliko wa Spika.
 
 

 

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Hashim Rungwe Jr., ni Muhitimu wa Sayansi ya Siasa(Political Science) kutoka Chuo cha Santa Barbara, jijini California. Amekuwa miongoni mwa waasisi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kitanzania jijini St. Petersburg, nchini Urusi, na kuongoza Jumuiya hiyo kama Katibu Mkuu na baadae Makamu Mwenyekiti (2002 - 2005). Amekuwa msaidizi wa masuala ya kiufundi katika kampeni ya Mh. Josh Lynn katika uchaguzi wa mwanasheria mkuu wa kitongoji cha Santa Barbara mwaka 2009. kwa sasa ni muasisi mshiriki, na Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, USA. Unaweza kumuandikia kupitia [email protected]

Related posts

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.