Bunge lapokea taarifa ajali ya Mv. Sky Get, abiria 113 hawajulikani walipo

Bungeni
Bungeni

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

BUNGE la Tanzania muda mfupi limepokea taarifa fupi ya ajali ya Meli ya Mv. Sky Get iliyotokea jana eneo la Chumbe nje kidogo ya Zanzibar. Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu jumla ya watu 113 waliokuwa katika meli hiyo hawajulikani walipo hadi sasa na juhudi za kuwatafuta bado zinafanywa.

Taarifa zimesema hadi sasa maiti 31 zimepatikana na kutambuliwa na ndugu, huku majeruhi 146 wameokolewa katika ajali hiyo wakiwa hai wakiwemo watalii 14. Jana zoezi la uokoaji lililazimika kusitishwa baada ya hali ya hewa kuwa mbaya eneo la ajali na zoezi hilo linaendelea tena leo.

Baada ya Bunge kupokea taarifa hiyo limelazimika kutoa posho za wabunge wote za siku moja na zitapelekwa Zanzibar kusaidia waliokumbwa na ajali hiyo. Spika wa Bunge Anne Makinda ameahirisha tena shughuli za bunge hadi kesho ili kutoa muda ya wawakilishi hao wa wananchi kuungana na wahanga wa ajali hiyo.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

Leave a Reply

Your email address will not be published.