Breaking News; Ajali juu ya ajali Zanzibar, hadi sasa 250 waokolewa kwenye ajali ya Meli ya Spice

Picha ya meli hiyo ikiwa imezama (Picha na Ahmed Muhamed Ahmad zanzinet)
Picha ya meli hiyo ikiwa imezama (Picha na Ahmed Muhamed Ahmad zanzinet)

TAARIFA ambazo zimetumwa na mmoja wa mashuda, kutokea Zanzibar, anasema ajali nyingine ya gari imetokea na watu watatu wamekufa papo hapo kati ya wananchi ambao wanaelekea eneo la Nungwi kuangalia ndugu zao waliopata ajali kwenye Meli ya Spice Islanders.

Na taarifa za sasa zinaeleza, watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na Vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo huko Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja. Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kasi za Zanzibar ambazo ilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.

Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwanja vya Maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kwa sasa Serikali inasafirisha maiti zote na majeruhi kuelekea Uwanja wa Maisara mjini, hivyo ndugu, jamaa na marafiki wasiendelee kwenda eneo la tukio Nungwi.

Jiunge nasi kwenye social media
Facebook
Instagram
Youtube
Twitter

About The Author

Joachim Ernest Mushi, Kitaaluma ni mwanahabari muhitimu (Uandishi-2006) wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (IJMC) kwa sasa Shule Kuu ya Uandishi na Mawasiliano. Nimekuwa mwandishi wa habari za uchunguzi (Gazeti la Kulikoni & Thisday), Mwandishi mwandamizi Gazeti kongwe la Kiongozi, Mhariri wa Makala mwanzilishi wa Gazeti la Jambo Leo. Kwa sasa ni Mhariri Mkuu Kiongozi wa Thehabari.com, nchini Tanzania.

Related posts

22 Comments

 1. Abrahman Ali

  Tupowe watu wa Zanzibar na watanzania kiujumla juu ya msiba huu wa kitaifa, poleni wafiwa naiyo kazi ya Allah, Mungu aziweke roho za marehemu pahala pema peponi, Amiin

  Reply
  1. Abrahman Ali

   Mie ni mzanzibar ambaye kwasasa niko shinyanga mgodini na haturuhusiwi kuingia sim, naomba taarifa yoyote itakayojiri mniarifu kupitia email yangu, niko field

   Reply
    1. Idrissa khamis

     mbona siamini kama hiyo picha ni yakikweli au bado unatumia picha nyengine ambazo hazihusiki.mimi ni mmoja ambae alihudhuria katika tukio hilo na hivi sasa nipo maisara kusikiliza idadi ya watu ni wangapi lakin bado hakuna lolote linaloendelea isipokua blablaa tu.Je unashindwa kusema ni abiria wangapi ambao wakuemo katika meli hiyo?mimi naweza kusema kwani najua meli za pemba zinavyo sheheni abiria na mizigo.

     Reply
 2. Idrissa khamis

  Nikweli kwamba ni ajali mbaya sana amboyo imetokea katika bandari yetu lakini bado wananchi wanahamu yakujua ni abiria wangapi ambao walikuemo katika meli hiyo bado kuna utata mkubwa katika familia mbalimbali juu ya ajali hiyo.Tumepata kujua idadi ndogo(250) ya watu ambao wameokolewa lakin bado mamia ya abiria yapo katika kina cha maji.Je ni watu wangapi ambao wameshapoteza maisha yao kiukweli bado hali ni mbaya sana hapa zanziibar kama watu waliookolewa ni hao basi kuna 350 bado wapo katika maafa haya bado tunahitaji msada wa hali ya juu.

  Reply
 3. Idrissa khamis

  bado nipo katika viwanja vya maisara ambapo mamia ya wananchi wanashuhudia na kuziangali maiti ambazo zinapitishwa na ambao wameokolewa lakini bado serikali hajatoa idadi kamili nii abiri wangapi waliokuemo katika meli hiyo.nimezungumza na mmoja kati ya waliokua wanaokoa watu katika ajali hiyo “bado hali ni mbaya sana kwani bado watu ni wengi sana ambao hajaokolewa katika ajali hiyo japokua serikali inasema imefanikiwa kuokoa lakini bado hali mbaya”

  Reply
 4. Beda

  Kwa kweli inasikitisha sana kwa kutokea ajali za mara kwa mara hapa tanzania. Tunasikitika sana kwa kupoteza ndugu zetu, marafiki zetu, watoto wetu, baba na mama zetu katika ajali za kizembe ambazo zaweza kuepukika. Hasa kinachonipa hasira zaidi ni kwa nini vyombo hivi havikaguliwi mara kwa mara na mamlaka husika? au ndo kusema wameajiriwa kukaa ofisini kwa kupiga soga na kusoma magazeti? Jamani innaniuma sana.

  poleni sana wafiwa, Mwenyezi Mungu awatie nguvu na hekma na busara katika kipindi hiki cha majonzi makubwa.
  Jina la Bwana lihimidiwe.

  Beda S. Msacky

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published.