Baadhi ya maaskofu wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiinyanyua juu picha ya Rais Magufuli, baada ya kuipaka mafuta na kuiombea.
Askofu wa Good Newsfor All Ministry, Dkt. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari wakati madhehebu mbalimbali hapa nchini walipomuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nchi, pamoja na kumpongeza kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam. Kushoto ni Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist jijini na katikati ni Askofu Ernest Sumisumi wa kanisa hilo.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiongozwa na Askofu wa Good Newsfor All Ministry, Dkt. Charles Gadi (katikati), wakiimba wimbo wa amani wakati wa kumuombea Rais Dk. Magufuli na Taifa.
Askofu Filbert Mbepera (wa pili kuli) wa Kanisa la EAGT, akiombea amani nchi.
Askofu Ernest Sumisumi (wa pili kushoto) wa Kanisa la Baptist akiiombea ramani ya Tanzania pamoja na picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Askofu wa Good Newsfor All Ministry, Dkt. Charles Gadi na Askofu Filbert Mbepera (kuli), wakiyabariki mafuta ya kupaka picha ya Rais, Dk. Magufuli.
Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist akiipaka mafuta picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Askofu John Sambuki (wa pili kulia) wa Victory Gospel Assemble a.k.a Furahini Katika Bwana, akiiombea bendera, wakati wa hafla hiyo.
Maaskofu na baadhi ya watumishi wa madhehebu hayo ya dini ya Kikristo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maombi hayo.
Na Lilian Lundo – Maelezo
ASKOFU wa Good Newsfor All Ministry Dkt. Charles Gadikwa niaba ya dini na madhehebu mbalimbali hapa nchini wamempongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Dkt. Gadi ametoa pongezi hizo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).
“Tunamshukuru Mungu kwa kumuinua Rais ambaye ameonyesha nia na kuwa mstari wa mbelekupigana na biashara hiyo haramu, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la dawaya kulevya ni kubwa na lenye madhara makubwa sana kwa watanzaniawengi haswa vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa,” alifafanua Dkt. Gadi.
Aliendelea kwa kusema kuwa, Vijana wengi wamepoteza maisha , kuharibika akili, kupata magonjwa ya kuambukiza, kupotezamalengo ya kimaisha kwa sababu ya dawa hizo. Vile vile dawa hizo zimeleta fedheha kwa Taifa kutokana na Vijana wengi wa Kitanzania kuwepo katika magereza mbalimbali Duniani huku wengine wakisubiriadhabuya kunyongwa.
Aidha amempongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kuimarisha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwakumteua Kamishna ambaye atasimamia Mamlaka hiyo na anaamini kwamba kwa neema ya Mungu ataweza kumsaidia kikamilifu Rais Magufuli katika kutimiza azma yake ya kukomeshabiashara hiyo.
Wakati huo huo, Dkt. Gadi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuianzisha vita hiyo dhidi ya matumizi ya dawa kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam. Vile vile amewapongeza waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari kwa kutoa habari zinazosaidia katika upambanaji wabiashara hiyo.
Dkt. Gadi amewataka viongozi wa Dini kuungana bega kwa bega na Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa maadili kwa vijana ili kuepukana na uovu wa dawa za kulevya nchini.