Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akutana na wananchi wa Dar es salaam na kupokea malalamiko ya migogoro inayohusu ardhi katika mkoa wa Dar es salaam tarehe 22 na 23, septemba, 2015 kuanzia saa 4.00 asubuhi makao makuu ya Wizara hiyo.
Katika siku ya tarehe 22 septemba 2015 Waziri amepokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya kinondoni na tarehe 23 septemba 2015 atapokea malalamiko ya wananchi kwa manispaa ya Temeke na Ilala.
