Sharti la Ndoa Bila Cheti cha Kuzaliwa Latenguliwa na Rais Magufuli

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017. Mhe. Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari …

Mbunge Tanga Amuangukia Waziri Mwijage Juu ya TBS

   Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutotoa kibali cha ubora unaohitajika na hivyo kusitisha  uzalishaji.   Mkurugenzi Uzalishaji wa kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Vivek Pandey  kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na shirika la viwango Tanzania (TBS) kutokutoa kibali cha ubora unaohitajika wa kiwanda hicho  na hivyo …

Mwakilishi Mkazi wa UN Tanzania Aridhishwa na Utekelezaji wa Miradi Kagera

  Umoja wa Mataifa kupitia Mkurugenzi wake Mkazi nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez umetembelea, kukagua na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na umoja huo Mkoani Kagera ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani (618,000 USD) zimetolewa ili kufadhili na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Elimu na Afya pia na miradi ya kijamii. Bw. Alvaro Rodriguez ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Mashirika matatu ya Umoja wa Maifa …

Halotel Yawezeshwa Wafanyabiashara Kutangaza Biashara Bure kwa Simu

    KUELEKEA kukua kwa teknolojia ya mawasiliano nchini kumeendelea kuwawezesha watanzania kupata nafasi ya kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na mitandao ya simu, Mtandao wa simu wa Halotel umezindua huduma itakayo wawezesha wateja wake ambao ni wafanya biashara kuweza kutangaza biashara zao bure kwa kutumia huduma mpya iliyozinduliwa na kampuni hiyo inayojulikana kama Halo SAINI. huduma hii inamuwezesha mteja …

Watendaji wa Serikali Waagizwa Kulinda Wawekezaji Wazawa

SERIKALI imewataka viongozi wa kisiasa pamoja na watendaji wa serikali kutotumia madaraka yao vibaya kuwanyanyasa na kuwasumbua wawekezaji wazawa waliowekeza ndani ya nchi. Aidha viongozi hao wametakiwa kuwaheshimu na kuwajengea mazingira rafiki yatakayowawezesha kufanya biashara zao kwa amani ili kuweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira kwa vijana. Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na …

Kampuni ya Manji Yatamka Kumuunga Mkono Rais Magufuli

  Ralph akielezea jinsi uongozi ulivopanga mikakati ya kuboresha kampuni zilizopo na kuanzisha nyinginezo nchini na nje ya nchi.   Suleiman Msuya KAMPUNI ya Quality Group Limited (QGL), imesema inaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.   Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo …