Makaburi 22 ya Watu Wenye Ualbino Tanzania Yafukuliwa

TANGU kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini  Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana. Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. …

Mbunge Ridhiwani, Madiwani Chalinze Waibana CHALIWASA

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Chalinze, wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) kwa kushindwa kusambaza maji ili kuondoa kero hiyo. Alisema mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini unasuasua. Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani lililofanyika Lugoba. Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado …

Maofisa Wakuu Jeshi la Polisi Kukutana Dodoma Kujipanga…!

              Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi MAOFISA Wakuu wa Jeshi la Polisi  wanatarajia kukutana mkoani Dodoma kuanzia Jumatatu tarehe 27-29/03/2017 katika kikao kazi cha siku tatu kujadili na kupanga mikakati mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu na wahalifu hapa nchini. Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake, Msemaji wa Jeshi la Polisi,  Kamishna Msaidizi wa …

TTCL KUZALISHA DOLA MIL 50

    WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi miwili Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kuhakikisha kuwa inapata Dola za Kimarekani milioni 50 ili kuongeza pato kwa Kampuni na Taifa kwa ujumla kupitia Mkongo wa Taifa. Akitoa agizo hilo, wilayani Bukoba mkoani Kagera, Waziri Prof. Mbarawa amesema agizo hilo limetokana na Serikali kuongeza masafa kwa kampuni …

Nape Aonja Joto ya Jeshi la Polisi, Wamzuia Kuzungumza na Wanahabari…!

  ALIYEKUWA Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Mnauye leo ameonja joto la jiwe la Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam baada ya kumzuia kuzungumza na vyombo vya habari alipotaka kuzungumza yamoyoni baada ya kuvuliwa nafasi yake ya uwaziri. Jeshi la Polisi lilizuia waandishi wa habari kuingia katika Hoteli ya Protea ya jijini Dar es Salaam sehemu …

WAZIRI MBARAWA AITAKA BODI YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADILIAJI MAJENZI KUJITANUA ZAIDI Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano, Prof Makame Mbarawa akizungumza (2) Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kwenye Mkutano wa mashauriano baina ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Majenzi unaofanyika kwa siku mbili kuanzia jana, katika Ukumbi wa Rock City Mall …