Filamu 132 Kuoneshwa Tamasha la Filamu Nchi za Majahazi, ZIFF 2017

  UONGOZI wa waandaaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), mapema leo Mei 19.2017, wametangaza rasmi filamu zilizochaguliwa kwa mwaka huu na ambazo zitaoneshwa kwenye tamasha hilo msimu wa 20, hapo Julai 8-16-2017. Akizungumza na waandishi wa Habari Jijii Dar e Salaam, Mkurugenzi wa ZIFF, Bw. Fabrizio Colombo amesema kuwa, jumla ya filamu 132, zimeweza …

Ndege Vita za China Zaizuia Ndege ya Marekani

  NDEGE mbili za kijeshi za China zimeizuia ‘vibaya’ ndege ya Marekani kulingana na jeshi la Marekani. Ndege hiyo inayohusika na kufanya uchunguzi, ilikuwa katika safari yake ya kutaka kugundua mionzi katika anga ya kimataifa iliopo mashariki mwa bahari ya China. Ndege hiyo ilikuwa imetumiwa kugundua ushahidi kuhusu majaribio ya kinyuklia ya Korea Kaskazini. China imekuwa ikituhumu vitendo vya Marekani …

Mkutano Mkuu wa Vijana Kimataifa Kufanyika Arusha kwa Siku 7

    AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari Mratibu wa Mkutano Mkuu Kivuli wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa, Tajiel Urioh alisema mkutano huo ni maigizo ya vitendo ya baraza kuu la Umoja wa Mataifa ambapo vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 30 kutoka sehemu mbalimbali wanapata fursa ya kujifunza Diplomasia, Uongozi na namna Umoja Wa Mataifa unavyofanya kazi. Bw. …

MUHAS WATAKIWA KUWEKA MAKAZI YA KUDUMU OLOLOSOKWAN

CHUO Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimetakiwa kuhakikisha kwamba wanatumia vyema kijiji cha kidigitali cha Ololosokwan katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na uwezo mkubwa katika tiba mtandao. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya wakati akifunga warsha ya siku 2 ya tiba mtandao iliyofanyika chuoni hapo. Warsha …

Rais Donald Trump Aipa Tanzania Dola Milioni 526

SERIKALI ya Marekani kupitia ofisi ya rais Donald Trump imetangaza kupatia Tanzania ufadhili wa kukabilana na virisu vya ukimwi. Marekani, ambayo siku chache zilizopita ilitangaza kusimamisha ufadhili wake kwa wizara ya afya nchini Kenya, imeipa Tanzania kitita cha dola milioni 526. Kitita hicho kutoka mfuko wa PEPFAR, kitatumika kufanikisha mpango wa kutoa huduma kwa zaidi ya watu milioni 1.2 wanaoishi …

Trump Aunga Mkono Mpango wa Nyuklia wa Iran

IKULU ya Whitehouse nchini Marekani imeendeleza mpango wa kuipunguzia vikwazo Iran licha ya rais Donald Trump kuukosa mpango huo. Kuondolewa kwa vikwazo ni miongoni mwa makubaliano ya kinyuklia yalioafikiwa 2015 chini ya aliyekuwa rais Barrack Obama pamoja na mataifa mengine matano yenye uwezo mkubwa duniani. Bwana Trump ameelezea makubaliano hayo kuwa mabaya zaidi. Hatahivyo wizara ya fedha nchini humo iliwawekea …