KAMPUNI ya mawasiliano ya simu ya Halotel, imezindua kampeni mpya ya Switch to Halotel, yenye lengo la kuwahamasisha Watanzania kujiunga na Mtandao huo sambamba na kuzindua utaratibu wa wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea wateja wa Mtandao huo katika maeneo yote nchi nzima mjini na vijijini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo iliyofanyika katika soko la Makumbusho lililoko …
Moto Mkubwa Waua Watu Kadhaa London
MOTO huo katika jengo la Grenfell Tower ulianza majira ya saa 01:16, saa za Uingereza. Hata hivyo Idara ya wazima moto jijini London ilituma malori 40 ya kuzima moto huo. Watu kadha wamefariki baada ya moto mkubwa kuteketeza jengo refu usiku wa kuamkia leo mjini London. Wazima moto bado wanakabiliana na moto huo katika jumba la Grenfell Tower, …
Kiongozi Wabunge wa Congress Anusurika Kuuwawa kwa Risasi
KIONGOZI wa Wabunge waliowengi wa Bunge la Congress nchini Marekani, Steve Scalise amenusurika kufa baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa alipokuwa akihudhuria mazoezi ya mchezo wa baseball miongoni mwa wabunge. Yamkini watu wawili wamejeruhiwa, katika kile mashuhuda wanasema kuwa kisa cha umiminunaji wa risasi katika jimbo la Virginia mapema leo Jumatano. Seneta wa Republican, Rand Paul, anasema kuwa alisikia mlio …
Max Malipo Yazaliwa Upya, Maxcom Africa Public Ltd
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom Africa Dr. Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyona ambayo inaiwezesha Kampuni kumilikiwa na Umma wa watanzania. Akiongea na Wanahabari Dr. Ulomi amesema kwamba Kuanzia Sasa Kampuni ya Maxcom Africa itatambulika kwa Jina la Maxcom Africa Public Limited Company (Maxcom Africa PLC). Kampuni hii maarufu kwa jina …
DC Hai ‘Avamia’ Shamba la Mbowe, Ang’oa Mfumo wa Umwagiliaji…!
Mkuu wa Wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Hai katika lango la kuingilia katika shamba la Kilimo cha Kisasa la Mboga Mboga la Kilimanjaro Vegees Ltd lililopo Nshara Machame. Mkuu wa wilaya ya Hai,akiwaongoza wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya Hai, pamoja na askari Mgambo wakiingia katika shamba …
Milioni 85 Kujenga Madarasa Shule ya Msingi Hondogo, Kibamba
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 14, 2017 Ameeleza dhamira yake kuhusu ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya Msingi Hondogo iliyopo katika Kata ya Kibamba. MD Kayombo ametoa ufafanuzi huo ofisini kwake alipokuwa akitoa tathmini ya ziara yake aliyoifanya katika Shule ya Msingi Hondogo Jana tarehe 13 June 2017. Katika ziara hiyo ambayo Mkurugenzi aliambatana na Mchumi Mkuu wa …