UNIC Yakutana na Wanafunzi Mbalimbali Kujadili Mkutano wa Bahari

                    KITUO cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) leo kimekutana na baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali na vijana kuzungumzia masuala mbalimbali yaliojiri katika mkutano wa Mkubwa wa Kimataifa (The Ocean Conference, United Nations) uliofanyika jijini, New York kuanzia Juni 5-9, 2017 na kukutanisha nchi na wadau anuai wa Bahari. …

WADAU WA JOTOARDHI WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

    Meneja Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania, Mhandisi Kato Kabaka akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo.   Ofisa misitu Mkuu Kitengo cha Nishati Mbadala, Paul Kiwele akiongea wakati wa Warsha ya wadau wa Jotoardhi iliyofanyika Dar es Salaam leo.     Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na …

Chuo cha Ufundi Arusha na DIT Wasaini Kushirikiana

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika(wa tatu kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology(DIT)Profesa Preksedia Marco Ndomba(wa pili kulia) wakisaini mkataba wa mashirikiano (MoU) kati ya taasisi hizo mbili. MoU imejikita kwenye ushirikiano wa Utafiti,  Taaluma, kubadilishana wataalamu, ziara za kitaaluma kwa wanafunzi.   Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC), Dk Richard Masika …

UWT Yaungana na Rais Magufuli Kuhusu Makinikia, Mikataba ya Madini

  JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) inaunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli na kupongeza jitihada zake za kupambana na aina zote za ubadhirifu, dhulma na unyonyaji uliobainika kwenye mikataba ya uchimbaji na usafirishaji madini, na hivyo kuhakikisha maliasili za Taifa zinatumika kwa manufaa ya watanzania wote. Pia, Umoja wa Wanawake Tanzania unatoa pongezi kwa …

Balozi Mahiga Ampokea Mkuu Mpya wa Shirika la UN Kuendeleza Viwanda Tanzania

    Na Stella Vuzo WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga leo amepokea hati za utambulisho za mwakilishi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda nchini Tanzania (UNIDO) wizarani kwake jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Mahiga alisema kiongozi huyo, aitwaye Dr. Stephen Kargbo kutoka nchini Sierra …