Jumuiya ya Waislam DMV Yafuturisha nchini Marekani…!
Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Canada, Col. Aldoph Mutta (kushoto) akimlaki Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Wilson Masilingi siku ya Jumamosi June 17, 2017 siku Mhe. Balozi alipokua mgeni rasmi kwenye futari ya pamoja inayoandaliwa na Jumuiya ya Waislam DMV (TAMCO) Silver Spring, …
ZIFAHAMU BAADHI YA SEHEMU ZA KITALII JIJINI DAR ES SALAAM
Na Jumia Travel Tanzania UMAARUFU wa Dar es Salaam kwenye shughuli za kibiashara umelifanya jiji hili kuwa vigumu kwa watu kuvizingatia vivutio vyake vya kitalii. Watu wengi huvifahamu kwa kuviona tu lakini bila ya kujua kihistoria sehemu hizo zina maana sana na wageni huja wakitokea nchi mbalimbali kujifunza. Ukiachana na ufukwe wa Coco Beach unaopatikana pembezeni mwa bahari ya hindi …
UNESCO Yatahadharisha Ongezeko la Jangwa…!
Nchi yetu. Nyumba zetu. Mustakabali wetu. Hii lazima iwe kauli mbiu yetu leo – hasa katika mapambano dhidi ya kuenea kwa jangwa. Mchango wa mabadiliko ya mazingira katika uhamiaji na makazi ya watu uko wazi duniani kote. Idadi kubwa ya ‘wakimbizi wa mazingira’ sasa huwasilishwa kama moja ya matokeo makubwa ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuenea kwa jangwa. …
UNIC yataka wahitimu Academic International kutojiingiza katika dawa za kulevya
KITUO cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimewaonya wanafunzi wa ‘Academic International Primary School’ waliohitimu Darasa la Saba kutojiingiza katika dawa za kulevya, kwani ni eneo linaloharibu kwa kasi maisha ya vijana wengi kupitia makundi. Ushauri huo umetolewa jana na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo …