Wenyeviti, Watendaji wa Kata na Mitaa Dar Washiriki Mafunzo

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Wenyeviti wa Mitaa, Watendaji wa Kata na Mitaa yatakayofanyika kwa siku nne katika ukumbi wa Manispaa ya Ubungo.   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akielezea lengo la mafunzo muda mchache kabla ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kufungua mafunzo ya kuwajengea …

Wanakijiji Kakola Waudai Fidia Mgogi wa Bulyanhulu

WAKAZI wa Kijiji cha Kakola, Kata ya Bulyanhulu, Wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga wameazimia kufanya maandamano yasiyo na ukomo kushinikiza mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu kuwalipa fidia zao. Wakizungumza kwenye kongamano la Kijiji hicho lililofanyika jana juni 20,2017, wakazi hao wamepanga kupeleka kero zao Jijini Dar es salaam kwa Rais John Pombe Magufuli pamoja na kufanya maandamano ya kufunga barabara kushinikiza kulipwa …

Makamu wa Rais, Suluhu Azindua Ugawaji Vifaa tiba kwa Wanawake Tanzania

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Samia Suluhu Hassan amezindua zoezi la ugawaji wa mabeseni yenye vifaa tiba 1000 kwa ajili ya wanawake wajawazito Tanzania bara na Zanzibar. Vifaa hivyo vimetolewa na Serikali ya Kuwait kupitia Ubalozi wake hapa nchini, Lengo la mpango huo ni kukabiliana na vifo vya watoto na wanawake wajawazito nchini. Tukio hilo pia …

HakiElimu Wazinduwa Kampeni Maalumu Kuhamasisha Elimu ya Mtoto

    TAASISI ya HakiElimu leo kwa kushirikiana na asasi wadau wengine watetezi masuala anuai ya kijamii wamezinduwa kampeni maalumu ya kuhamasisha ufanikishaji wa elimu ya mtoto wa kike, huku ikiiomba Serikali kupitia wizara husika kukamilisha mchakato wa kumruhusu mtoto wa kike aliyepata ujauzito aendelee na masomo baada ya kadhia hiyo. Hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo imefanyika leo katika …