Rais JK na Mrema wasakata rhumba dodoma

JK akicheza na Mwenyekiti wa TLP na Mbunge wa Vunjo Mh. Augustine Lyatonga Mrema wakati wa mnuso wa kuwapongeza wabunge kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo. Kulia ni Mzee Yusuf ambaye kundi lake la Jahazi Modern Taarab lilikuwa likitumbuza.

Diamond atikisa London

Msanii aliyeingia kwenye game kwa safu kali hasa kwa kibao chake maarufu ‘Mbagala’,ameonekana kupata mafanikio makubwa sana mwaka huu. Licha ya kuwa msanii pekee kutoka Tanzania kuteuliwa kama msanii chipukizi katika Tuzo za MTV Base, Diamond ameonekana kukubalika vilivyo na mashabiki ndani na nje ya nchi. Msanii huyo hivi karibuni alipata nafasi ya kwenda kupiga shoo Uingereza ambapo ilisadikika kuwa …

T-Pain, Mims and Gyptian in Bongo

Katika kile kinachoonekana kuwa Dar-Es-Salaam ni mji wa maraha tarehe 27 ya mwezi huu Dar-es-salaam kutawaka moto kwani tamasha linalofuata litamaliza kiu ya burudani ya muziki kwa mashabiki wa wasanii na muziki wa nje.

Basata kubana maadili kwa wasanii

Basata imekuja mkakati mwingine wa kuhakikisha kuwa wanaikomboa tasnia ya sanaa dhidi ya kupambana na maadili machafu katika filamu hususan tabia ya kuvaa na kukaa nusu uchi na kufanya mambo ya aibu yasiyovumilika. Basata inajipanga kuweka kanuni za adhabu ambazo zitadhibiti maadili katika filamu na wasanii wake kupitia mashirikisho husika. Marais wa mashirikisho hayo ambao ni Symon Mwakifwamba (Filamu), Adrian …

Ray C ang’aka kuhusu Bangi

Msanii mahiri wa muziki wa Bongo flava nchini, Rehema Chalamila, a.k.a Ray C hivi karibuni aligeuka mbogo baada ya kuulizwa na Paparazi kuhusu tuhuma za yeye na mpenzi wake wa zamani, Waziri Isaac Makuto, ‘Lord Eyez’ kutumia bangi na kana kwamba ndiyo chanzo cha kuachana kwao.