Na Ismail Ngayonga, MAELEZO KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) inakusudia kuongeza mabehewa 4 kwa ajili ya abiria wanaotumia huduma ya usafiri wa treni kutoka kituo cha Dar es salaam hadi Pugu kufikia mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu. Ongezeko hilo litafanya mabehewa kufikia 20 kutoka 16 yaliyopo sasa hali itakayoongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya usafiri huo kwa abiria …
Samia Awataka Wakadiriaji Majenzi Kuwa Waadilifu
Na Frank Shija-Maelezo WATAALAMU wa Ukadiriaji Majenzi wameelezewa kuwa ni kada muhimu katika kukabiliana na tatizo la rushwa pamoja na matumizi mabaya ya rasilimali za umma katika sekta ya ujenzi dunia kote. Hayo yamebainishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu wakati akimuwakilisha Rais John Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa mkutano …
Askofu Gadi Amuunga Mkono Rais Magufuli…!
Na Sheila Simba, Maelezo ASKOFU Dk. Charles Gadi ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli, katika mchakato wake wa kuhamishia Serikali makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma kwani ni uamuzi wa kijasiri na unapaswa kuungwa mkono. Akizungumza na waandishi wa habari jijini dare Es Salaam Askofu Gadi amesema kuwa jitihada zinazofanywa na Rais magufuli ni kubwa kwani jitahada …
Serikali Yampongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo
Na Benedict Liwenga-WHUSM SERIKALI imempongeza Mwandishi wa Kamusi ya Ukristo Padre Jordan Nyenyembe pamoja na wadau wengine waliohusika katika kufanikisha uandishi wa Kamusi hiyo. Pongezi hizo zimetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni katika Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Bibi. Lily Beleko ambaye alimwakilisha mgeni rasmi Mhe. Waziri Nape Nnauye …
Vyuo Vilivyopokea Fedha Vyapewa Siku Saba Kurejesha
Na: Lilian Lundo na Sheila Simba – MAELEZO Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako ametoa siku saba kuanzia Agosti 17, 2016 kwa vyuo vikuu kurejesha fedha zilizopokea ambazo ni za wanafunzi ambao hawapo chuoni. Prof. Ndalichako ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya taarifa la zoezi la uhakiki wa wanafunzi …